• HABARI MPYA

  Saturday, July 21, 2012

  AZAM KUFA NA KUPONA LEO, SIMBA HESHIMA TUUU


  Azam FC

  Na Prince Akbar
  SIMBA inacheza mechi ya mwisho ya Kundi A, Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame dhidi ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), mchezo ambao unatarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua na wakati huo huo Azam watacheza na Tusker ya Kenya katika Kundi B.
  Timu zote, Vita inayofundishwa na kocha wa zamani wa Yanga, Raoul Jean Pierre Shungu na Simba inayofundishwa na Mserbia Milovan Cirkovick, zimekwishafuzu Robo Fainali, lakini mchezo wa leo unaweza tu kurekebisha tu msimamo wa kundi hilo, timu ipi iwe ya pili na ipi iwe ya tatu,
  Simba SC
  Simba SC walijihakikishia kufuzu Robo Fainali jana baada ya vinara wa kundi hilo, URA kuichapa Ports ya Djibouti mabao 3-1. Ports iliyoanza kwa kufungwa 7-0 na AS Vita, juzi pia ilifungwa na Simba mabao 3-0 hivyo kuaga mashindano kwa kupoteza mechi zote .
  Shujaa wa Simba katika mchezo huo, alikuwa mshambuliaji mpya kutoka Ruvu Shooting ya Pwani, Abdallah Juma aliyeingia kuchukua nafasi ya Amri Kiemba mwanzoni mwa kipindi cha pili aliyefunga mabao mawili dakika za 60 na 73 na Felix Mumba Sunzu Jr. aliyefunga moja kwa penalti dakika ya 64 
  Kinara wa mabao Simba SC; 
  Abdallah Juma 'Dullah Mabao'
  Dakika 45 za kipindi cha kwanza zilimalizika bila nyavu za Ports kutikisika, na katika kipindi hicho Sunzu, mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia, alipoteza nafasi tatu za wazi mno, za kufunga mabao akiwa amebaki yeye na kipa, Kalid Ali Moursal.
  Mabadiliko yaliyofanywa na kocha Mserbia, Milovan Cirkovick kipindi cha pili kuwaingiza Juma Nyosso kuchukua nafasi ya Haruna Shamte, Abdallah Juma aliyechukua nafasi ya Kiemba na baadaye Uhuru Suleiman kuchukua nafasi ya Haruna Moshi ‘Boban’ yaliisaidia Simba.
  Kiungo wa Azam Gerorge
   Odhiambo 'Blackberry'
  Matokeo hayo, yanaifanya Simba iwe na pointi tatu baada ya kucheza mechi mbili na sasa inashika nafasi ya tatu kwenye Kundi A, nyuma ya URA yenye pointi tisa na AS Vita yenye pointi tatu na wastani mzuri wa mabao. Simba inamaliza na AS Vita ya DRC, mechi ambayo itakuwa kali kwa sababu timu zote zina pointi sawa.  
  Mechi za Kundi C zilimalizika jana na Atletico wameongoza kundi, Yanga wa pili na APR wa tatu, timu zote zikifuzu Robo Fainali.
  Mechi za Kundi B zinahitimishwa pia leo kwa mchezo utakaotangulia saa 8:00 mchana kati ya Tusker ya Kenya na Azam FC ya Dar es Salaam.
  Tusker iliyotoka sare ya bila kufungana na Mafunzo ya Zanzibar juzi, imelifanya kundi hilo lizidi kuwa gumu na katika mchezo wa leo, timu itakayoshinda moja kwa moja itaungana na Mafunzo kutinga Robo Fainali.
  Hatima ya Mafunzo kucheza au kutocheza Robo Fainali inashikiliwa na mechi hiyo, kwani iwapo timu hizo zitatoka sare ya kuanzia mabao 2-2 zitakwenda zote Nane Bora na wawakilishi wa Zanzibar watarejea nyumbani.


  MISIMAMO YA MAKUNDI KOMBE LA KAGAME:
  KUNDI A:
                       P   W  D  L   GF      GA     GD     Pts
  URA             3   3   -    -    8         2         6         9
  AS Vita        2   1   -    1   8         3         5         3       
  Simba           2   1   -    1   3         2         1         3
  Ports             3   -    -    3   1         10      -9       -

  KUNDI B:
                       P   W  D  L   GF      GA     GD     Pts
  Mafunzi        2   -    2   -    1         1         -         2
  Azam FC      1   -    1   -    1         1         -         1       
  Tusker FC    1   -    1   -    -         -         -         1

  KUNDI C
                       P   W  D  L   GF      GA     GD     Pts
  Atletico         3   2   1   -    7         -         7         7
  Yanga           3   2   -    1   9         3         6         6
  APR             3   1   1   1   7         2         5         4       
  Waw             3   -    -    3   -         19      -19     0
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM KUFA NA KUPONA LEO, SIMBA HESHIMA TUUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top