• HABARI MPYA

    Friday, July 27, 2012

    KIATU CHA DHAHABU KAGAME SASA NI BALAA


    Kiiza akiwa amebebwa na Bahanuzi jana
    Na Prince Akbar
    VITA ya kuwania kiatu cha dhahabu cha Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame imezidi kupambana moto, baada ya John Raphael Bocco ‘Adebayor’ wa Azam FC na Hamisi Kiiza ‘Diego’ wa Yanga kutimiza mabao matano kila mmoja, hivyo kulingana na Said Bahanuzi ‘Spider Man’ anayeshika nafasi ya pili, nyuma ya Taddy Etikiama na AS Vita ya DRC, mwenye mabao sita.
    Wachezaji wote hao wanne, watakuwa na fursa ya kuongeza mabao yao Jumamosi, Bocco, Kiiza na Bahanuzi wakicheza fainali kati ya Yanga na Azam, wakati Taddy akiiongoza AS Vita katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu, dhidi ya APR ya Rwanda.    
    John Bocco wa Azam
    Wengine waliomo kwenye kinyang’aniyo hicho ni Suleiman Ndikumana wa APR mwenye mabao mabao matatu, ambaye pia anaweza kuongeza mabao yake katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu keso.
    Abdallah Juma ‘Dullah Mabao’ wa Simba SC timu yake imetolewa akiwa ana mabao mawili sawa na Leonel St Preus wa APR, Didier Kavumbagu wa Atletico, Feni Ali na Robert Ssentongo wa URA.

    WANAOONGOZA KWA MABAO:
    Taddy Etikiama                AS Vita        6
    Said Bahanuzi                 Yanga SC    5
    Hamisi Kiiza                     Yanga SC    5
    John Bocco                      Azam FC     5
    Suleiman Ndikumana       APR            3
    Abdallah Juma                 Simba SC   2
    Leonel St Preus               APR            2
    Didier Kavumbagu           Atletico        2
    Feni Ali                            URA            2
    Robert Ssentongo            URA            2 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIATU CHA DHAHABU KAGAME SASA NI BALAA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top