Tetesi za Jumanne magazeti Ulaya


JUVE WATENGA PAUNI MILIONI 70 KUMNASA ROBIN VAN PERSIE

KLABU ya Juventus imepanga kutumia pauni Milioni 70 kwa mshambuliaji wa Arsenal, Robin van Persie, mwenye umri wa miaka 28. Kiwango hicho kinajumuisha ada ya uhamisho na mshahara wa mchezaji huyo, lengo ni kuhakikisha wanazipiga bao Manchester United na Manchester City kuinasa saini ya Van Mabao.
MSHAMBULIAJI wa Liverpool, Andy Carroll hataki kwenda West Ham United. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23, ameripotiwa kuwaambia rafiki zake, ataondoka Anfield tu kurejea Newcastle United.
Robin van Persie joined Arsenal in 2004
Van Persie alijiunga na Arsenal kutoka Feyenoord mwaka 2004
Liverpool pia imekataa pauni Milioni 13 kutoka Manchester City kwa ajili ya kumuuza beki wake wa kati, Daniel Agger, mwenye umri wa miaka 27.
The Hammers pia wanataka kuimarisha safu yao ya ulinzi kwa kusajili wachezaji watatu, kutoka Aston Villa, James Collins, Mallorca, Ivan Ramis Sebastian Boenisch ambaye ni mchezaji huru.
MABINGWA wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Chelsea wanatayarisha dau la mwisho la pauni Milioni 7.5 kwa ajili ya winga mwenye umri wa miaka 21 wa Wigan Athletic, Victor Moses.
MABINGWA wa Hispani, La Liga, Real Madrid wameiambia Tottenham hawatatoa pauni Milioni 40 wanazotaka kwa ajili ya kiungo Luka Modric, mwenye umri wa miaka 26.

RIO AJUTIA UFEDHULI WAKE

BEKI wa Manchester United, Rio Ferdinand, mwenye umri wa miaka 33, anajutia tweet yake iliyomponza kuadhibiwa na Chama cha Soka England.
KOCHA wa Tottenham, Andre Villas-Boas ameelezea ahueni yake baada ya kubainika winga Gareth Bale, mwenye umri wa miaka 23, hajaumia sana baada ya kugongwa na kiungo na Liverpool, Charlie Adam.

AGUERO AGEUKA BUBU

KOCHA Msaidizi wa Manchester City, na mchezaji wa kimataifa wa England, David Platt, mwenye umri wa miaka 46, amerudisha saa nyuma kufanyisha mazoezi ya basikeli, ambayo yalimfanya Sergio Aguero ashindwe kuzungumza.