• HABARI MPYA

  Tuesday, May 15, 2018

  MANCINI KOCHA MPYA ITALIA, AMFIKIRIA TENA BALOTELLI

  KOCHA wa Italia, Roberto Mancini amesema atazungumza na mshambuliaji Mario Balotelli ambaye hajaitwa muda mrefu juu ya uwezekano wa kurejeshwa timu ya taifa.
  Akizungumza wakati wa kutambulishwa kwake mjini Florence leo, Mancini amesema; "Mario ni mchezaji wa Italia. Dhahiri tutazungumza. Ni mmoja wa wachezaji tutakaowatazama upya,"amesema.
  Balotelli hajachezea Italia tangu Kombe la Dunia mwaka 2014, lakini alicheza chini ya Mancini klabu za Inter Milan na Manchester City ingawa wakati wote waliingia kwenye mizozo.

  Kocha mpya wa Italia, Roberto Mancini amesema atazungumza na Mario Balotelli juu ya kumrejesha kikosini PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Mancini amechukua nafasi ya Gian Piero Ventura, aliyefukuzwa mwezi Novemba baada ya Azzurri kushindwa kufuzu Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza katika miongo sita. 
  Mabingwa hao mara nne wa Kombe la Dunia, Italia wapo katika kiwango duni mno kisoka kihistoria, kwa sasa wakishika nafasi ya 20 kwenye viwango vya FIFA baada ya kufungwa 1-0 jumla na Sweden katika mchezo wa mchujo wa kuwania nafasi ya Urusi. 
  Walitolewa katika hatua ya makundi tu ya Kombe la Dunia mara zote 2010 na 2014, ingawa wamefanya vyema kwenye michuano ya Ulaya, wakifika fainali fainali mwaka 2012 na Robo Fainali mwaka 2016.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MANCINI KOCHA MPYA ITALIA, AMFIKIRIA TENA BALOTELLI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top