• HABARI MPYA

  Tuesday, May 15, 2018

  FAINALI LIGI YA MABINGWA ULAYA KUONYESHWA BURE

  FAINALI ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya Liverpool na Real Madrid itaonyeshwa bure kwenye YouTube Mei 26, mwaka huu kutoka Uwanja wa NSK Olimpijs mjini Kyiv, Ukraine.
  BT Sport imekubali kuonyesha bure mechi za mwisho za michuano ya klabu Ulaya kwa wote, kikosi cha Jurgen Klopp kikimenyana na wakali wa Zinedine Zidane Mei 26.
  Fainali ya Europa League pia baina ya Atletico Madrid na Marseille Mei 16 pia itaonyeshwa bure.
  BT Sport ilivutia watazamaji Milioni 6.5 kwenye fainali ya mwaka jana kati ya Real Madrid na Juventus, lakini inatarajia idadi hiyo itaongezeka mwezi huu kutokana na kuhusisha timu ya England.

  Mwanasoka Bora wa Dunia, Cristiano Ronaldo anatarajiwa kuiongoza Real Madrid katika Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Liverpool kesho PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: FAINALI LIGI YA MABINGWA ULAYA KUONYESHWA BURE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top