• HABARI MPYA

  Wednesday, September 11, 2019

  KAGERE APIGA MBILI, RWANDA YAICHAPA 7-0 SHELISHELI KUFUZU QATAR 2022

  RWANDA imefuzu hatua ya makundi ya kuwania tiketi ya Kombe la Dunia 2022 Qatar kwa ushindi wa kishindo wa 7-0 dhidi ya Shelisheli jana Uwanja wa Nyamirambo mjini Kigali.
  Mabao ya Amavubi jana yalifungwa na Djihad Bizimana dakika ya 16, Meddie Kagere dakika ya 27 na 51, Jacques Tuyisenge dakika ya 28 na 34, Yanick Mukunzi dakika ya 57 na Muhadjir Hakizimana dakika ya 79.
  Maana yake, Rwanda inayofundishwa na kocha mzalendo Vincent Mashami inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 10-0 baada ya kushinda 3-0 kwenye mchezo wa kwanza Alhamisi a wiki iliyopita, mabao ya Hakizimana 31, Mukunzi 35 na Kagere 81.

  Rwanda inaungana na washindi wengine 13 wa hatua ya awali kuungana na timu 26 za viwango vya juu vya ubora wa soka barani Afrika kwa ajili ya hatua ya makundi, ambayo yatakuwa 10.
  Washindi wa kwanza wa kila kundi watamenyana baina yao kupata wawakilkishi watano wa Afrika kwenye Fainali zijazo za kombe la Dunia nchini Qatar 2022.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KAGERE APIGA MBILI, RWANDA YAICHAPA 7-0 SHELISHELI KUFUZU QATAR 2022 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top