• HABARI MPYA

    Thursday, September 26, 2019

    CHELSEA V MAN UNITED, LIVERPOOL V ARSENAL RAUNDI YA NNE CARABAO

    Manchester United itamenyana na Chelsea katika Raundi ya Nne ya Kombe la Ligi England, maarufu kama Carabao Cup Uwanja wa Stamford Bridge mjini London.
    Hiyo ni baada ya kuitoa Rochdale kwa penalti 5-3 kufuatia sare ya 1-1 kwenye mchezo wa Raundi ya Tatu usiku wa jana Uwanja wa Old Trafford. 
    Nayo Liverpool baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Milton Keynes Dons Uwanja wa MK mjini Buckinghamshire, sasa itamenyana na Arsenal Uwanja wa Anfield.

    Kocha wa Chelsea, Frank Lampard atawapokea Manchester United katika Raundi ya Nne ya Carabao Cup 

    Marco Silva amepangwa dhidi ya timu yake ya zamani, Everton dhidi ya Watford. 

    RAUNDI YA NNE YA KOMBE LA LIGI ENGLAND, AU CARABAO CUP

    Everton vs Watford
    Aston Villa vs Wolves
    Man City vs Southampton
    Burton vs Leicester 
    Chelsea vs Manchester United
    Oxford United vs Sunderland
    Liverpool vs Arsenal
    Crawley Town vs Colchester
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CHELSEA V MAN UNITED, LIVERPOOL V ARSENAL RAUNDI YA NNE CARABAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top