• HABARI MPYA

  Wednesday, September 11, 2019

  HISTORIA NA TAKWIMU ZAIBEBA YANGA SC DHIDI YA ZESCO UNITED

  Na Dominick Salamba, DAR ES SALAAM
  SIKU ya jumamosi ni siku ambayo wawakilishi wa Tanzania bara katika michuano ya Klabu Bingwa barani Afrika Yanga SC watakuwa katika uwanja wa Taifa kukipiga dhidi ya vijana wa ZESCO United kutoka nchini Zambia huku Yanga wakiwa na mambo manne muhimu katika mchezo huo.
  Moja ni kuweka historia katika miaka ya karibuni kuingia katika hatua ya makundi katika michuano hii mikubwa barani afrika kwani ni zaidi ya miaka 10 yanga haijapata nafasi hii,hivyo endapo watapata matokeo mazuri hasa katika mechi hii ya kwanza katika uwanja wa nyumbani itakuwa ni mwanga mzuri kuelekea kutinga katika hatua ya Makundi.
  Pili ni kuwa karibu kujizolea zaidi ya dola laki 4 ambazo watapatiwa na shirikisho la soka barani Afrika endapo wataingia hatua hiyo,si jambo dogo ni mkwanja mrefu sana ambao Yanga sc hawatakiwi kuukosa hata kidogo.
  Tatu ni kuwapa raha wapenzi na mashabiki wao ili kuendelea kujenga umoja na mshikamano na kuendeleza hamasa ambayo imeendelea kutamalaki katika siku za hivi karibuni.
  Nne ni kuendelea kuzitendea haki nafasi 4 ambazo Tanzania bara imezipata katika kuwakilisha michuano ya kimataifa kwa maana ya mbili katika michuano ya klabu bingwa na mbili katika michuano ya shirikisho.
  Kuelekea mchezo huo mgumu na muhimu yapo mambo baadhi ambayo kwa ujumla wake yanaipa nafasi klabu ya Yanga kupenya katika makundi dhidi ya ZESCO United kama ifuatavyo.

  (KUANZISHWA KWAKE.*
  Yanga ilianzishwa mwaka 1935, February 1.
  Wakati ZESCO United ilianzishwa Mwaka 1974.

  SEHEMU TIMU ZILIPO:
  Yanga inapatika Tanzania- Kariakoo Jijini Dar es Salaam.
  ZESCO wao wanapatikana Zambia katika mji wa Ndola".

  *JEZI WANAZOTUMIA:
  Yanga wanatumia Kijani kwa Nyumbani, na njano ugenini.
  ZESCO wao wanatumia rangi ya machungwa nyumbani na kijani ugenini.

  VIWANJA WANAVYOTUMIA:
  Yanga inatumia uwanja wa Taifa (Kwa Mkapa) wenye uwezo wa kuingiza mashabiki Zaidi ya Elfu 60,000..
  ZESCO wao wanatumia uwanja wa Taifa wa Zambia (Levy Mwanawasa) wenye uwezo wa kuingiza zaidi ya watu 49,000.

  MAKOCHA:
  Yanga ipo chini ya  Kocha wao Mwinyi Zahera. akisaidiwa na Noel Mwandila huku kocha wa makipa akiwa Peter Manyika.
  ZESCO wao wapo chini ya  Kocha Mkuu George Lwandamina.

  MAFANIKIO:
  Yanga hadi hivi sasa ina  jumla ya mataji 27 ya ligi kuu Tanzania bara..
  ZESCO wao wanamataji 7 ya ligi Kuu nchini Zambia.

  MAFANIKIO KIMATAIFA:

  1_KLABU BINGWA AFRIKA:
  Yanga imeshiriki mara 11,huku nafasi za juu kuwahi kufika Yanga Ni hatua ya makundi 1998, na miaka mingine kuishia hatua za awali, raundi za kwanza na raundi ya pili.
  ZESCO wao katika michuano hii wameshiriki mara 5, huku mwaka 2016 wakiishia hatua ya Nusu fainali, kabla ya mwaka 2018 kuishia hatua ya makundi.

  KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA:
  Yanga wameshiriki mara 4. 2007 raundi ya 14, 2008 raundi ya kwanza, 2011 hatua za awali, 2016 hatua ya makundi..
  ZESCO wao katika michuano hii wameshiriki mara 3, huku 2017 wakiishia hatua ya robo fainali.

  WATANI WA JADI:
  Yanga wao watani zao Ni Simba ambao huaminika kuwa Ni watani wakubwa Sana hapa Tanzania na Afrika kwa ujumla,na mchezo wa Yanga sc na Simba ni miongoni mwa Derby kubwa 5 barani Afrika na ni Derby yenye mvuto mkubwa kwa mashabiki wa soka.
  ZESCO wao watani zao wakubwa ni Nkana FC, Power Dynamos, pamoja na Napsa Stars.

  MASHABIKI:
  Yanga ina mashabiki zaidi ya Millioni 20 Tanzania na  Afrika Mashariki, Mashabiki hawa wanaitwa "WANANCHI" na Wana kaulimbiu Yao Inaitwa "DAIMA MBELE, NYUMA MWIKO"
  ZESCO pia Ni Miongoni Mwa vilabu vyenye mashabiki wengi nchini Zambia Wanajiita "ZESCOLO" na kauli mbiu yao "NI ZAIDI YA KLABU".
  Ukipitia kwa ufasaha utakugundua mambo makubwa mawili juu ya timu hizi.
  Kwanza klabu ya Yanga SC ni kongwe sana ukilinganisha na ZESCO huku ikiwa ina mtaji mkubwa sana wa mashabiki ambao wakitimiza majukumu yao basi itakuwa na faida kubwa kwenye mchezo wao wa nyumbani kwa kuongeza hari ya wachezaji wao kiasi kwamba wajitoe kwa bidii na kuleta matokeo mazuri kwa timu yao..
  Pili ni kwamba Yanga SC imeshiriki mara nyingi zaidi michuano ya Afrika kwa maana ya klabu bingwa na shirikisho jambo ambalo linawapa uzoefu wa kutosha katika michuano hata uku Zesco wakijivunia hatua ya Robo fainal ambayo waliifikia uko nyuma..
  Kwa ujumla wake Yanga SC wana kila sababu ya kupata matokeo uku kazi kubwa ikianza kufunywa na Viongozi na mashabiki kuhakikisha ule msemo wa kuwa shabiki ni mchezaji wa 12 uwanjani unakuwa na maana na kuleta tija kwa upande wao.
  Ni mechi ngumu ila ni kipimo kizuri kwa Yanga SC na nina uhakika watapata matokeo kwani wana wachezaji wazuri ambao bado wana safari kubwa katika maish ya soka,kikubwa ni benchi la ufundu kupitia ubora na udhaifu wa timu ya Zesco uku wakipanga kikosi ambacho kitaweza kufanya kile ambacho wengi tunataraji.
  Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki Klabu ya Yanga SC!

  (Dominick Salamba ni  mchambuzi wa soka anapatikana pia kupitia katika Akaunti yake ya instagram kama@dominicksalamba)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HISTORIA NA TAKWIMU ZAIBEBA YANGA SC DHIDI YA ZESCO UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top