• HABARI MPYA

  Monday, January 18, 2016

  'YELSTIN' WA SIMBA SC AFARIKI DUNIA, MAZISHI JIONI YA LEO KISUTU

  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limetuma salamu za rambirambi kwa klabu ya Simba SC, kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Kamati ya Muda ya klabu hiyo, kuanzia mwaka 1997-1999, Suleiman Said ‘Yelstin’ (pichani kulia).
  Yelstin aliyeiongoza Simba SC wakati wa mgogoro mkubwa miaka hiyo, amefariki jana mjini Dar es Salaam na anatarajiwa kuzikwa jioni ya leo makaburi ya Kisutu Jijini.
  Suleiman alipewa jina la utani Yelstin na wanachama wa Simba SC na kutokana na misimamo yake wakati huo kufananishwa na aliyekuwa Rais wa Urusi, Boris Yeltsin.
  "TFF kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu nchini inawapa pole familia ya Seleman Said ‘Yelstin’ ndugu jamaa, marafiki, uongozi na wanachama wa klabu ya Simba kufuatia kifo hicho, na kusema wako pamoja katika kipindi hiki cha maombelezo,".
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: 'YELSTIN' WA SIMBA SC AFARIKI DUNIA, MAZISHI JIONI YA LEO KISUTU Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top