• HABARI MPYA

    Friday, January 22, 2016

    VITA YA KUWANIA TIKETI YA KOMBE LA CAF YAFIKIA PATAMU; KESHO NI BURKINA FASO NA SIMBA MOROGORO, JUMAPILI YANGA NA FRIENDS RANGERS TAIFA

    RATIBA KOMBE LA AZAM SPORTS HD – TFF
    Januari 23, 2016
    Burkina Faso Vs Simba SC (Jamhuri, Morogoro)
    Pamba Vs Toto Africans (Kirumba, Mwanza)
    Ndanda FC Vs Mshikamno (Nagwanda, Mtwara)
    Januari 24, 2016
    Yanga SC Vs Friends Rangers (Taifa, Dar es Salaam)
    Njombe Mji Vs Prisons (Amaan, Njombe)
    Stand Untd Vs Mwadui FC (Kambarage, Shinyanga)
    Januari 25, 2016
    Kagera Sugar Vs Rhino Rangers (Mwinyi, Tabora)
    Panone FC Vs Madini (Ushirika, Moshi)
    African Lyon Vs Azam FC (Karume, Dar es Salaam)
    Januari 26, 2016
    Mtibwa Sugar Vs Abajalo FC (Jamhuri, Morogoro) Lipuli Vs JKT Ruvu (Wambi, Mafinga)
    African Sports Vs Coastal U (Mkwakwani, Tanga)
    Geita Gold Vs Mgambo JKT (Nyankumbu, Geita)
    Januari 27, 2016
    Singida United Vs Mvuvuma (Namfua, Singida)
    Februari 1, 2016
    Wenda FC Vs Mbeya City (Sokoine, Mbeya)
    Simba SC inawania kurejea kwenye michuano ya Afrika kupitia Kombe la TFF

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    VITA ya kuwania nafasi ya kuiwakilisha Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho la Soka Afrika imfikia patamu; wakati Raundi ya Tatu Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup itakapoendelea wikiendi hii.
    Kesho Jumamosi michezo mitatu itachezwa, mjini Morogoro Burkinfaso watawakaribisha Simba SC katika uwanja wa Jamhuri mjini humo,  Pamba watawakaribisha Toto Africans uwanja wa CCM Kirumba, huku Ndanda FC watakua wenyeji wa Mshikamno FC katika uwanja wa Nagwanda Sijaona Mtwara.
    Jumapili michuano hiyo itaendelea kwa michezo mitatu pia, jijini Dar es salaam Young Africans watawakaribisha Friends Rangers uwanja wa Taifa, Njombe Mji watakua wenyeji wa Tanzania Prisons uwanja wa Amani Njombe, huku Stand United wakiwakaribisha Mwadui FC katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
    Michuano hiyo itaendelea Jumatatu, Kagera Sugar wakiwa wenyeji wa Rhino Rangers katika uwanja wa Ali Hassani Mwinyi mjini Tabora, Panone FC dhidi ya Madini uwanja wa Ushirika- Moshi na Africa Lyon wakiwa wenyeji wa Azam FC uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.
    Jumanne Mtibwa Sugar watawakaribisha Abajalo FC uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, Lipuli dhidi ya JKT Ruvu uwanja wa Wambi Mafinga, Africa Sports dhidi ya Coastal Union Mkwakwani jijini Tanga, na Geita Gold watakua wenyeji wa Mgambo Shooting katika uwanja wa Nyankumbu mjini Geita.
    Singida United watacheza dhidi ya Mvuvuma siku ya Jumatano katika uwanja wa Namfua mjini Singida, na mchezo wa mwisho utachezwa Februari Mosi katika ya Wenda FC dhidi ya Mbeya City uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
    Hadi sasa timu ya JKT Mlale pekee ndio imeshafuzu kwa mzunguko wa nne baada ya kuiondosha Majimaji kwa mabao 2-1, katia mchezo uliochezwa wiki iliyopita kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea. 
    Ikumbukwe bingwa wa Kombe la Azam Sports HD - TFF ataiwakilisha nchi kwenye Kombe la Shirikisho mwakani, huku bingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara atacheza Ligi ya Mabingwa Afrika.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: VITA YA KUWANIA TIKETI YA KOMBE LA CAF YAFIKIA PATAMU; KESHO NI BURKINA FASO NA SIMBA MOROGORO, JUMAPILI YANGA NA FRIENDS RANGERS TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top