• HABARI MPYA

    Monday, January 25, 2016

    AZAM FC YAIFANYA KITU MBAYA AFRICAN LYON MAWINDO YA TIKETI YA CAF 2017

    MATOKEO NA RATIBA KOMBE LA AZAM SPORTS HD – TFF
    Leo; Januari 25, 2016
    African Lyon 0-4 Azam FC (Karume, Dar es Salaam)
    Kagera Sugar 1-1 Rhino Rangers (Kagera imeshinda kwa penalti 4-2 Mwinyi, Tabora)
    Panone FC 3-1 Madini (Ushirika, Moshi)
    Januari 24, 2016
    Yanga SC 3-0 Friends Rangers (Taifa, Dar es Salaam)
    Njombe Mji 0-0 Prisons (Prisons imeshinda kwa penalty 5-3 Amaan, Njombe)
    Stand Untd 0-1 Mwadui FC (Kambarage, Shinyanga)
    Januari 23, 2016
    Burkina Faso 0-3 Simba SC (Jamhuri, Morogoro)
    Pamba 1-4 Toto Africans (Kirumba, Mwanza)
    Ndanda FC 5-0 Mshikamno (Nagwanda, Mtwara)
    MECHI ZIJAZO; 
    Januari 26, 2016
    Mtibwa Sugar Vs Abajalo FC (Jamhuri, Morogoro) Lipuli Vs JKT Ruvu (Wambi, Mafinga)
    African Sports Vs Coastal U (Mkwakwani, Tanga)
    Geita Gold Vs Mgambo JKT (Nyankumbu, Geita)
    Januari 27, 2016
    Singida United Vs Mvuvuma (Namfua, Singida)
    Februari 1, 2016
    Wenda FC Vs Mbeya City (Sokoine, Mbeya)
    Farid Mussa amefunga mabao mawili Azam FC ikiichapa 4-0 African Lyon leo Kombe la TFF Uwanja wa Karume
    AZAM FC imezifuata Simba na Yanga SC hatua ya 16 Bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports HD Federation Cup baada ya kuitandika mabao 4-0 African Lyon jioni ya leo Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
    Mabao ya Azam FC leo yamefungwa na Mudathir Yahya dakika ya pili, Farid Mussa dakika za tatu na 37 na Ame Ali ‘Zungu’ dakika ya 55.
    Mechi nyingine ya leo ya michuano hiyo ambayo itatoa mwakilishi wan chi kwenye Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF) mwakani, Panone FC imeifunga 3-1 Madini Uwanja wa Ushirika mjini Moshi, wakati Kagera Sugar imeshinda kwa penalti 4-2 baada ya sare 1-1 na Rhino Rangers Uwanja wa Mwinyi mjini Tabora.
    Kikosi cha Azam FC leo kilikuwa; Aishi Manula, Shomary Kapombe/Khamis Mcha dk46, Farid Mussa, Abdallah Kheri, Erasto Nyoni, Jean Baptiste Mugiraneza/Said Mourad dk67, Kipre Balou, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, John Bocco/Allan Wanga dk57, Ame Ally na Mudathir Yahya.
    African Lyon; Hamad Juma, Mandela Mgunda, Omary Salum/Kassim Simbaulanga dk46, William Otong, Hamadi Manzi, Baraka Jaffar, Hamisi Issa, Awadh Salum, Tito Okello, Raizam Hafidh/Hood Mayanja dk59 na John Simbeya/Abdallah Mguhi dk73.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC YAIFANYA KITU MBAYA AFRICAN LYON MAWINDO YA TIKETI YA CAF 2017 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top