• HABARI MPYA

    Saturday, January 23, 2016

    UGANDA WAPIGWA 1-0 NA ZAMBIA, SASA MGUU NJE, NDANI CHAN

    Chris Katongo (juu) ameifungia bao pekee Zambia ikiilaza Uganda 1-0 na kutinga Robo Fainali CHAN
    UGANDA inaangalia mlango wa kutokea kwenye Michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) baada ya kipigo cha 1-0 leo kutoka kwa Zambia katika mchezo wa Kundi D mjini Kigali, Rwanda.
    Bao lililoizamisha The Cranes leo limefungwa na mkongwe, Christopher Katongo dakika ya 41, akimalizia kazi nzuri ya Benson Sakala.
    Mchezo mwingine wa kundi hilo, Mali imeweka hai matumaini ya kusonga mbele baada ya kuilaza 1-0 Zimbabwe, bao pekee la Moussa Sissoko dakika ya 82.
    Zambia sasa inafuzu Robo Fainali kwa ushindi huo, wakati The Cranes itatakiwa kushinda dhidi ya Zimbabwe katika mchezo wa mwisho na kuimba Zambia iifunge Mali, ili Korongo wa Kampala wafuzu Robo Fainali kama washindi wa pili.
    Michuano hiyo itaendelea kesho kwa mechi za mwisho za Kundi A, wenyeji Rwanda wakimenyana na Morocco na Ivory Coast wakimaliza na Gabon.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: UGANDA WAPIGWA 1-0 NA ZAMBIA, SASA MGUU NJE, NDANI CHAN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top