• HABARI MPYA

  Tuesday, August 09, 2016

  PAUL WERE ATUA DENIZLISPOR SC YA UTURUKI MWAKA MMOJA

  WINGA wa kimataifa wa Kenya, Paul Were anatarajiwa kujiunga na klabu ya Denizlispor SC ya Daraja la Kwanza Uturuki kwa Mkataba wa mwaka mmoja.
  Were amefuzu majaribio katika timu hiyo baada ya kufanya nayo mazoezi katika kipindi cha kujiandaa na msimu mpya baada ya kuondoka FC Kalloni ya Ugiriki.
  "Nina furaha mambo mazuri yanatokea katika kazi yangu na nakaribia kusiani Mkataba wa mwaka mmoja Denjzlispor. Ni klabu yenye utamaduni sana na dira yao ipo wazi,"alisema.
  Were alimvutia kocha Karay Palaz katika maandalizi ya msimu mpya kutokana na ujuzi wake wa kui heza soka na kufikia uamuzi wa kumsajili.

  Denizlispor yenye maskani yake Denizil, Uturuki wanacheza mechi zao za nyumbani kwenye Uwanja wa Denizil Ataturk wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 19, 500. na watauanza msimu mpya wa 2016/17 kwa kumenyana na Bandirmaspor Agosti 21.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PAUL WERE ATUA DENIZLISPOR SC YA UTURUKI MWAKA MMOJA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top