• HABARI MPYA

    Wednesday, August 24, 2016

    TOTO AFRICANS YAANZA VYEMA LIGI KUU, YAITANDIKA MWADUI YA JULIO 1-0 KIRUMBA

    Na Mwandishi Wetu, MWANZA
    TIMU ya Toto African ya Mwanza imeanza vyema Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kushinda bao 1-0 dhidi ya Mwadui FC ya Shinyanga.
    Shukrani kwa mfungaji wa bao hilo pekee, Waziri Junior dakika ya 36 aliyemshinda mbio beki wa Mwadui na kufumua shuti dhaifu lililomshinda kipa na kutinga nyavuni. 
    Huo unakuwa mwanzo mzuri kwa kocha Rogasian Kaijage aliyechukua nafasi iliyoachwa wazi, John Tegete aliyeondolewa baada ya msimu uliopita – na mwanzo mbaya wa kocha wa Mwadui, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’.
    Waziri Junior ameifungia bao pekee Toto leo ikiilaza 1-0 Mwadui FC
    Mechi za ufunguzi za Ligi Kuu Jumamosi, Simba SC iliichapa Ndanda FC 3-1 Uwanja wa Taifa, Azam ililazimishwa sare ya 1-1 na African Lyon Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam, Ruvu Shooting iliifunga 1-0 Mtibwa Sugar uwanja wa Mabatini Mlandizi, Pwani na Stand United ikalazimishwa sare ya 0-0 na Mbao FC Uwanja wa Kambarage Jumamosi Prisons ikashinda ugenini 1-0 dhidi ya Maji Maji Uwanja wa Maji Maji, Songea wakati Jumapil Mbeya City ililazimisha sare ya 0-0 na Kagera Sugar Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.
    Ligi Kuu itaendelea Jumamosi wakati Mtibwa Sugar watakuwa wenyeji wa Ndanda FC Uwanja wa Manungu, Morogoro, Azam wataikaribisha Maji Maji na Prisons watakuwa wenyeji wa Ruvu Shooting Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
    Mechi nyingine za Jumamosi, Mbao watakuwa wenyeji wa Mwadui FC Uwanja wa Kirumba, Mwanza, JKT Ruvu watamenyana na Simba Uwanja wa Taifa, Kagera Sugar watamenyana na Stand United Uwanja wa Kambarage, wakati mabingwa watetezi, Yanga SC watacheza mechi ya kwanza Jumapili kwa kumenyana na African Lyon, siku ambayo pia Toto Africans watakuwa wenyeji wa Mbeya City Kirumba, Mwanza.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TOTO AFRICANS YAANZA VYEMA LIGI KUU, YAITANDIKA MWADUI YA JULIO 1-0 KIRUMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top