• HABARI MPYA

    Monday, August 22, 2016

    PHIRI: SOKA TULICHEZA, SEMA HAIKUWA BAHATI YETU

    Na Mwandishi Wetu, SHINYANGA
    KOCHA Mmalawi wa Mbeya City, Kinnah Phiri amesema kwamba walikosa bahati tu ya kufunga mabao wakitoa sare ya 0-0 jana na wenyeji Kagera Sugar Uwanja wa Kambarage, Shinyanga katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. 
    Phiri alisema timu yake ilicheza vizuri na kutengeneza nafasi nyingi, lakini ikashindwa kumalizia tu kwa kufunga na wazi ilikosa bahati katika mchezo huo.
    “Tulicheza vizuri, hatukuwa na bahati, mapungufu kadhaa tumeayaona  tutayafanyia kazi ili tuweze kuibuka na matokeo zaidi kwenye micheo inayofuata, asanteni sana  mmefanya vizuri”.
    Kocha Phiri wa kwanza kushoto katika benchi la Mbeya City kwenye moja ya mechi za msimu uliopita

    City ilianza  dakika 45 za mwanzo kwa mashambulizi makali  ikimiliki eneo la kiungo lilokuwa chini ya Kenny Ally na kufakikiwa kulifikia mara kadhaa lango la Kagera Sugar, lakini umakini kwenye safu ya ushambuliaji ulihitimisha dakika hizo za mwanzo timu zote zikiwa 0-0.
    Kipindi cha pili kocha Kinnah Phiri alifanya mabadiliko ya kuwatoa, Joseph Mahundi, Rajabu Isihaka na Salvatory Nkulula na nafasi zao kuchukuliwa na Michael Kerenge, Ramadhani Chombo na Ditram Nchimbi  mabadiliko ambayo yalikuja kuongeza ushai  safu ya ushambuliaji lakini mpaka dakika 90 zinakamilika hakukuwa na bao lolote.
    Mechi nyingine za ufunguzi za Ligi Kuu, Simba SC iliichapa Ndanda FC 3-1 Uwanja wa Taifa, Azam ililazimishwa sare ya 1-1 na African Lyon Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam, Ruvu Shooting iliifunga 1-0 Mtibwa Sugar uwanja wa Mabatini Mlandizi, Pwani na Stand United ikalazimishwa sare ya 0-0 na Mbao FC Uwanja wa Kambarage Jumamosi Prisons ikashinda ugenini 1-0 dhidi ya Maji Maji Uwanja wa Maji Maji, Songea.
    Ligi Kuu itaendelea Jumatano kwa Toto Africans kuikaribisha Mwadui Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, wakati Jumamosi Mtibwa Sugar watakuwa wenyeji wa Ndanda FC Uwanja wa Manungu, Morogoro, Azam wataikaribisha Maji Maji na Prisons watakuwa wenyeji wa Ruvu Shooting Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
    Mechi nyingine za Jumamosi, Mbao watakuwa wenyeji wa Mwadui FC Uwanja wa Kirumba, Mwanza, JKT Ruvu watamenyana na Simba Uwanja wa Taifa, Kagera Sugar watamenyana na Stand United Uwanja wa Kambarage, wakati mabingwa watetezi, Yanga SC watacheza mechi ya kwanza Jumapili kwa kumenyana na African Lyon, siku ambayo pia Toto Africans watakuwa wenyeji wa Mbeya City Kirumba, Mwanza.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PHIRI: SOKA TULICHEZA, SEMA HAIKUWA BAHATI YETU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top