• HABARI MPYA

    Monday, August 22, 2016

    RASIMU ZA DONDOO ZA MKUTANO WA DHARURA YANGA SC AGOSTI 6

    Mwenyekiti wa Yanga, Yussuf Manji (wa pili kushoto) akizungumza na wadau mbalimbali wa klabu hiyo hivi karibuni kwenye Mkutano Mkuu wa dharula ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam

    1. SALA ZA UFUNGUZI

    1.1. Sala ya Wakristo ilisomwa.

    1.2. Sala ya Waislam ilisomwa.

    2. UFUNGUZI WA MKUTANO ULIFANYWA NA MWENYEKITI, WA YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB SAA 5 ASUBUHI. 

    3. KUPITISHWA KWA AJENDA KULITOLEWA NA MWENYEKITI, WA YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB SAA 5:30 ASUBUHI.
    3.1. Wanachama walikubaliana kuipitisha Ajenda.

    4. MASUALA YA SOKA – YALISOMWA NA MWENYEKITI, WA YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB.
    4.1. Msimu uliopita, Klabu: 
    4.1.1. Ilipata ushindi wa Ngao ya Jamii; 
    4.1.2. Ilikuwa Mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom 2015 /2016     Vodacom;
    4.1.3. Ilikuwa mshindi wa Kwanza wa Kombe la FA;
    4.1.4. Ilifikia raundi ya tatu ya Ligi ya Mabingwa na ikapoteza mchezo wa marudiano nchini Misri; na
    4.1.5. Ilifikia hatua ya Kombe la Shirikisho na Hatua ya Makundi baada ya karibu miaka 20 kupita bila kufikia hatua hiyo ya makundi ya Mashindano ya Kimataifa ya Bara la Afrika. 
    4.1.6. Wakati Klabu ya Young Africans Sports ni klabu pekee ambayo inaiwakilisha Jamhuri ya Tanzania katika mashindano ya Kimataifa, yaani katika Hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika  (CAF Confederation Cup Group Stage),  kuna changamoto kubwa mbele kwa Klabu katika kufikia hatua ya mbele zaidi katika maendeleo ya soka na inategemewa kuchukua miaka isiyopungua minne ili kufika katika hatua za nusu fainali za Mashindano ya Bara la Afrika na miaka ipatayo sita ya juhudi za kuweza kufika katika fainali za mashindano hayo. 

    4.2. Mwenyekiti, aliwafahamisha Wanachama kwamba pamoja na kushindwa katika mashindano hayo ya Afrika mwaka huu, lakini imani kubwa ya Wanachama na vitega uchumi vyao katika Yanga vinaonyesha kwamba hatimaye baada ya miaka kumi Klabu inaonyesha mwelekeo mzuri. 

    4.3. Mwenyekiti, kwa niaba ya Klabu, alielezea kufurahishwa na hatua za serikali, wakati wa mchezo dhidi ya TP Mazembe, kwa kuhakikisha kunakuwa na mazingira ya amani katika Uwanja wa Taifa, kwa kuondoa gharama za malipo ya uwanja na kwa kuzuia njama za Shirikisho la Soka nchini (TFF) kutaka kuweka kuifanya Klabu ilipe kodi ambazo hazikuwa na msingi.

    4.4. Mwenyekiti, aliendelea kwamba serikali iliunga mkono kwa kuruhusu Klabu kuwa na mchezaji wa 12, yaani wapenzi wa soka walioingia bure kuitazama mechi dhidi ya TP Mazembe ambapo walijitokeza kwa wingi licha ya kwamba Yanga haikushinda mchezo huo.  Kitendo hicho kiliifanya Klabu kuonyesha umoja na uzalendo wa Tanzania, jambo ambalo lilikuwa muhimu katika kuipa moyo timu.

    4.5. Mwenyekiti, aliongeza kusema kwamba katika mechi iliyofuatia dhidi ya Medeama SC kutoka Ghana, baada ya Rais wa TFF kusema kwamba shirikisho lake lingesimamia michezo yote ya Kimataifa ya timu za soka za Tanzania, Klabu ililazimika kuwatoza kiingilio mashabiki japokuwa kilikuwa cha chini.  Hata hivyo, Yanga ilitoa ombi kwamba fedha zilizopatikana kutokana na kiingilio, zitunzwe na uongozi wa Uwanja wa Taifa chini ya Wizara ya Michezo na kuilipa Yanga fungu lake kwa cheki.

    Ombi la Yanga lilikubaliwa na Wizara ya Michezo na licha ya makusanyo ya Sh. Milioni 118.2 kutoka kwenye viingilio, kitu cha kushangaza ni kwamba Klabu ilipata Sh. Milioni 59.2  tu (pamoja na kuondolewa kwa VAT) na licha ya kuomba kuweko mashine za kieletroniki za kutolea risiti (EFD) kutoka Wizara ya Michezo, TFF, na magari ya wagonjwa kutoka Muhimbili ili Klabu iweze kudai sehemu ya kodi, vitu hivyo havikutolewa na Yanga haiwezi kurudisha gharama za VAT zilizotokana na kodi ambazo zingekuwa Sh. Milioni 10.71 za ziada kwa Klabu.

    4.6. Mwenyekiti, pia alionyesha kushangazwa kwake kwa nini TFF haionyesha msimamo wa kuunga mkono mafanikio ya Klabu kama ambavyo mashirikisho ya nchi nyingine yanavyofanya.  Akielezea hilo, alitoa mfano kwamba;

    4.6.1. Rais wa TFF katika mkutano wake na Waandishi wa habari alisema kwamba mchezo wa TP Mazembe, shirikisho lingekuwa na wajibu wa kusimamia matayarisho ya mechi zote za Kimataifa za Yanga. (Kiambatisho cha 1 cha Taarifa ya Rais wa TFF iliyotolewa na kupitishwa);

    4.6.2. Mwenyekiti, wa Young Africans alikubali kuingia kwa shirikisho hilo kwa niaba ya Klabu, kwamba TFF ibebe gharama za matayarisho yote wakati wa kuikaribisha Medeama SC, na gharama zilizotokana na safari ya Yanga kwenda Ghana – jumla ya Sh. Milioni 170, bado hazijalipewa na TFF.  Yanga ilibidi kulipa fedha hiyo kwani ingejikuta ikifungiwa na CAF.  (Kiambatisho cha 2 cha Taarifa ya Yusuf Manji na Gharama zote Husika iliyotolewa na kupitishwa);

    4.6.3. Mwenyekiti, aliwaeleza Wanachama kwamba baada ya kuchaguliwa kwake mara ya kwanza mwaka 2013 Yanga ilijiandikisha katika VAT tangu mwaka huo, hata hivyo, hadi sasa TFF haijailipa Klabu kuhusu tiketi za VAT, kukodisha uwanja, na kadhalika, lakini imekuwa ikiitumia VAT kwa kujinufaisha kama vile kukodisha nyumba, na kadhalika (kuhusu kodi).   Iwapo TFF ingefuata tu sheria za Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) na kukusanya mapato kutokana na fedha inayoingia na kutoka kwa msingi wa VAT, Klabu ingekuwa na Sh. Milioni 382 ambazo TFF inadai inazilipa TRA bila ya kuwepo ushahidi wa Klabu kuzidai fedha hizo kutoka TRA (Kiambatisho cha 3 cha VAT kutoka TFF kilichotolewa na kupitishwa);

    4.6.4. Mwenyekiti, aliwakumbusha Wanachama kwamba Katiba ya Yanga, na marekebisho yake kwa mujibu wa Mkutano Mkuu wa Wanachama uliofanyika mnamo 2013 na 2014 vililenga kuleta mabadiliko katika Katiba hiyo ikiwemo Kamati ya Utendaji iteuliwe na Mwenyekiti, na Makamu Mwenyekiti, ili kupunguza msuguano katika Klabu kama ilivyokuwa hapo nyuma kabla ya kuingia kwake katika Klabu, kati ya Mwenyekiti, na Makamu Mwenyekiti,, jambo ambalo lilisababisha Klabu kufungwa na Simba magoli 5 kwa 0, lakini mwaka huu magoli manne yakiwa tayari yamelipwa na Klabu dhidi ya Simba.  Hata hivyo, TFF iliandika ikipinga maamuzi ya Wanachama ikitoa sababu za kuchekesha za Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) wakati kuna Klabu zinazomilikiiwa na watu binafsi au taasisi mbalimbali ambazo hazina tatizo lolote, wakati ambapo Vilabu vya Wanachama viko tayari kumilikiwa kibinafsi. (Kiambatisho cha 4 cha barua TFF inayokataa kuafiki umauzi wa wanachama iliyotolewa na kupitishwa);

    4.6.5. Mwenyekiti, aliwasomea wanachama marekebisho yaliyokubaliwa ya Katiba ambayo yalikubaliwa wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Wanachama wa Yanga wa mwaka 2013, kwamba “… baada ya uchaguzi wa Mwenyekiti, na Makamu Mwenyekiti, kwa pamoja watateua Kamati ya Utendaji ambayo watakuwa na uwezo wa kuindoa au kuteua nyingine mpya” lakini ilikataliwa na TFF; na 

    4.6.6. Mwenyekiti, aliwasomea wanachama marekebisho yaliyokubaliwa wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Yanga wa Juni 1, 2014 ambapo ulikubali kuanzishwa kwa Kamati ya Nidhamu kama ilivyotakiwa na TFF kutokana na maelekezo kutoka FIFA ili Yanga iweze kushiriki katika Ligi Kuu lakini ikakataliwa na TFF.  Hili halikuifanya Yanga ionekane kupingana na Sheria za Fifa tu, lakini ikiwa haina chombo cha kushughulikia masuala la Klabu hiyo kuhusiana na nidhamu;

    4.6.7. Mwenyekiti, aliendelea kwamba mabadiliko yaliyofanywa na wanachama kwenye Katiba yao yalipelekwa hata kwa Msajili wa Michezo ambapo hadi leo ni miaka mitatu hadi minne imepita bila Klabu kujulishwa chochote, jambo ambalo linamshangaza Mwenyekiti, iwapo serikali inaweza kuruhusu taasisi kama vile za kisiasa au wadhamini kuendesha shughuli zao bila Msajili wa Michezo kutambua Klabu husika, ambapo Klabu haijawasilisha mahesabu yake kwa serikali kwa miaka minne sasa.

    4.6.8. Mwenyekiti, aliripoti kwa Wanachama kwamba Uchaguzi Mkuu wa Yanga unahitajika kuendeshwa na kusimamiwa na Kamati ya Uchaguzi ya Yanga hata kwa mujibu wa Katiba ya 2010 ambapo Yanga ilikuwa na bajeti yake kulingana na sera za Klabu.  Yanga imedhamiria kuhakikisha shughuli zake zina faida kwa wanachama wake na si mtu mwingine na ndiyo maana hatukukubali Uchaguzi Mkuu kufanywa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF kama ilivyotaka kwamba Yanga ililazimika kwanza kulipa Sh. Milioni 9 kwa ajili ya posho, tiketi za ndege na gharama za hoteli kwa maofisa wa TFF kutoka Kagera kuja Dar es Salaam, hii ni bila kujumuisha gharama halisi za uchaguzi.  Hata hivyo, Yanga iliendesha uchaguzi wake kwa gharama zake, uchaguzi uliokuwa huru na wa haki (chini ya Katiba ya 2010) kwa kutumia Sh. Milioni 10 katika muda wa siku 14.  (Kiambatisho cha 5 cha barua ya maelekezo ya TFF, barua ya TFF kuhusu posho na taarifa ya gharama za Yanga ambayo ilitolewa na kupitishwa);

    4.6.9. Hitimisho la Mwenyekiti, ni kwamba viongozi walioshindwa wa Yanga ambao sasa wanaiendesha TFF, wanataka kuiendesha Yanga au kuihujumu.  (Kiambatisho cha 6 cha Celestine Mwesiga akiishitaki Yanga, iliyotolewa na kupitishwa);

    4.6.10. Mwenyekiti, aliomba mwongozo kutoka kwa Wanachama katika kuendesha shughuli za Klabu kwani pamoja na Jerry Murro kupeleka ripoti ya njama za TFF na Msajili wa Michezo katika uchaguzi wa Yanga, hakuna mtu yoyote katika Klabu aliyehojiwa wala hakuna afisa yeyote wa TFF au Wizara ya Michezo aliyesimamishwa, hali inayoonyesha utendaji kazi wa serikali ya sasa. 

    Mwenyekiti, aliendelea kusema kwamba Klabu imefahamu kupitia vyombo vya habari kwamba Jerry Murro amesimamishwa katika shughuli za soka kwa mwaka mmoja, pamoja na kwamba msingi wa hukumu hiyo haujaletwa kwa Klabu kimaandishi.  Hivyo, Mwenyekiti, alishangaa kutokuwepo kwa fursa ya kujielezea katika soka la Tanzania.  

    Mwenyekiti, alisema kwamba kuna wakati anasema kwa niaba ya Klabu na kuna wakati anakuwa anasema mambo yake kama mtu binafsi.  Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jerry ana haki ya kujieleza kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na anapozungumza kwa niaba ya Yanga kama Mwenyekiti, yeye ndiye msemaji mkuu na kiongozi mkuu.

    Mwenyekiti, alitoa fursa kwa Wanachama kutoa maoni yao.

    Hakuna Mwanachama aliyetoa maoni yoyote.

    4.6.11. Mwenyekiti, aliwajulisha Wanachama kwamba kwa mara nyingine TFF ilikuwa imesaini bila ya idhini ya Yanga mkataba mpya wa kituo cha Televisheni cha Azam kurusha Matangazo ya Ligi Kuu ya Vodacom, jambo alilosema litapunguza idadi ya watu kuingia viwanjani.  Mwenyekiti, alisema kwamba ni kweli Ligi Kuu katika muundo wa sasa inamilikiwa na TFF, lakini Wachezaji na nembo ni mali ya Yanga na kwamba kuzitumia vitu hivyo kwa ajili ya kuingiza fedha ni jambo haramu na kwamba ufumbuzi utapatikana mahakamani ambapo TFF na Azam TV watabidi kujibu na kufidia hasara inayotokana na kupoteza mapato ya Klabu.

    Wanachama walikubaliana juu ya hilo kwa kauli moja.

    4.6.12. Mwenyekiti, alitoa ombi kwamba kama kuna uwezekano, akiwa Mwenyekiti, wa Yanga, bidhaa za Azam zisusiwe hadi mgogoro huo wa kisheria umalizike.

    Wanachama walikubaliana na hoja hiyo kwa kauli moja. 
    GONGA HAPA KUSOMA ZAIDI 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RASIMU ZA DONDOO ZA MKUTANO WA DHARURA YANGA SC AGOSTI 6 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top