• HABARI MPYA

    Saturday, August 27, 2016

    MANJI AWAJAZA ‘FWEZA’ WACHEZAJI YANGA, AUNDA NA KAMATI MPYA YA MASHINDANO

    Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
    MWENYEKITI wa Yanga SC, Yussuf Manji jana amekutana na wachezaji wa timu hiyo na kuwalipa posho zao za msimu uliopita – lakini pia ameunda Kamati mpya ya mashindano baada ya kujizulu kwa Isaac Chanji.
    Chanji, aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano na akaiwezesha klabu kutwaa mataji yote matatu msimu uliopita, kuifunga Simba mechi zote na kufuzu hatua ya makundi Kombe la Shirikisho alijiuzulu Mei mwaka huu. 
    Na leo Manji ametaja Kamati mpya chini ya Mwenyekiti, Mhandisi Paul Malume, ambaye pia anaingia kwenye Kamati ya Utendaji kama Mjumbe Mteule.
    Manji jana amekutana na wachezaji wa timu hiyo na kuwalipa posho zao za msimu uliopita

    Wajumbe wa Kamati hiyo ni Abdallah Bin Kleb, Mustafa Ulungo, Mhandisi Mahende Mugaya, Jackson Mahagi, Samuel Lukumay na Hussein Nyika.
    Wengine ni Athumani Kihamia wa Arusha, Felix Felician Minja wa Mwanza, Leonard Chinganga Bugomola wa Geita, Omar Chuma, Hussein Ndama, Hamad Ali Islam wa Morogoro, Yusuphedi Mhandeni, John Mogha, Beda Tindwa, Moses Katabaro na Roger Lemlembe.  
    Awali ya hapo, juzi usiku Manji alikutana na wachezaji wa Yanga na kuwalipa malimbikizo ya posho zao zote za msimu uliopita kutokana na kutwaa mataji yote matatu nchini, Ngao ya Jamii, Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC).      
    Maana yake wachezaji hao wataingia kwenye mechi ya kwanza ya Ligi Kuu dhidi ya African Lyon Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na ari mpya baada ya kuanza vibaya msimu kwa kufungwa kwa penalti 4-1 baada ya sare ya 2-2 kwenye mchezo ea Ngao ya Jamii mbele ya Azam FC Agosti 17, mwaka huu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MANJI AWAJAZA ‘FWEZA’ WACHEZAJI YANGA, AUNDA NA KAMATI MPYA YA MASHINDANO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top