• HABARI MPYA

    Tuesday, August 23, 2016

    NIGERIA WASOGEZA MBELE MECHI NA STARS

    SHIRIKISHO la Soka Nigeria (NFA), limesogeza mbele kwa siku moja mchezo kati ya timu ya taifa ya Nigeria ‘The Super Eagles’ na Tanzania ‘Taifa Stars’ ambako sasa utafanyika Septemba 3, 2016 badala ya Septemba 2, 2016 iliyotangazwa awali.
    Na Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa kesho anatarajiwa kutangaza kikosi ambacho atakiandaa maalumu kwa mchezo huo. Mkwasa amesema kwamba anatarajia kuita wachezaji 20 ambao atasafiri nao kwenda Nigeria kwa ajili ya mchezo huo.

    “Kutakuwa na mabadiliko kidogo katika kikosi nitakachotangaza. Kwanza watakuwa wachezaji 20 badala ya 24, pili wachezaji ambao nitawachukua ni tofauti tofauti maana wengine kwa sasa ni majeruhi,” amesema Mkwasa.
    Mchezo huo ni wa kukamilisha ratiba katika kundi G baada ya Misri kukata tiketi ya kucheza Kombe la Mataifa ya Afrika, fainali zitakazofanyika Gabon, mwakani. Katika kundi hilo, Chad ilijitoa hivyo kuathiri mbio za ushindani wa nafasi hiyo kwa timu za Tanzania na Nigeria.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NIGERIA WASOGEZA MBELE MECHI NA STARS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top