• HABARI MPYA

    Tuesday, August 30, 2016

    TANZANIA YAPANGWA NA ETHIOPIA NA RWANDA CHALLENGE

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    TANZANIA imepangwa Kundi B pamoja na Ethiopia, Tanzania na Rwanda katika michuano ya ubingwa wa wanawake kwa mataifa ya Afrika Mashariki na Kati. 
    Katibu wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Nicholas Musonye amewaambia Waandishi wa Habari katika mkutano wa utambulisho wa Challenge hiyo ya wanawake mjini kampala, Jumatatu kwamba Uganda watakuwa wenyeji wa michuano hiyo.
    Katika sherehe za utambulisho wa michuano hiyo iliyofanyika makao makuu ya Shirikisho la Soka Uganda (FUFA), Musonye alisema nchi saba zimethibitisha kushiriki Challenge hiyo ya kwanza ya wanawake, itakayofanyika Jinja.
    Mbali za Tanzania, Ethiopia na Rwanda Kundi A linaundwa na timu za Uganda, Kenya, Burundi, na Zanzibar na michuano itaanza Septemba 11 hadi 20, 2016.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TANZANIA YAPANGWA NA ETHIOPIA NA RWANDA CHALLENGE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top