• HABARI MPYA

    Saturday, August 27, 2016

    SIMBA KUENDELEZA UBABE LIGI KUU LEO?

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea leo, mchezo unaosubiriwa kwa hamu ukiwa baina ya Simba SC na JKT Ruvu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Huo unatarajiwa kuwa mchezo mkali na wa kusisimua, haswa ikizingatiwa kila timu imeboresha zaidi kikosi chake kutoka msimu uliopita.
    Na Simba SC inayofundishwa na Mcameroon, Joseph Marius Omog baada ya kuanza na ushindi wa 3-1 dhidi ya Ndanda wiki iliyopita leo itataka kuwadhihirishia wapenzi wake kwamba msimu huu imerejesha makali. 
    Mechi nyingine za leo Mtibwa Sugar watakuwa wenyeji wa Ndanda FC Uwanja wa Manungu, Morogoro, Azam wataikaribisha Maji Maji na Prisons watakuwa wenyeji wa Ruvu Shooting Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
    Mbao watakuwa wenyeji wa Mwadui FC Uwanja wa Kirumba, Mwanza, Kagera Sugar watamenyana na Stand United Uwanja wa Kambarage, wakati mabingwa watetezi, Yanga SC watacheza mechi ya kwanza kesho kwa kumenyana na African Lyon, siku ambayo pia Toto Africans watakuwa wenyeji wa Mbeya City Kirumba, Mwanza.
    Katika mechi za ufunguzi za Ligi Kuu mbali na Simba SC kuichapa Ndanda FC 3-1 Uwanja wa Taifa, Azam ililazimishwa sare ya 1-1 na African Lyon Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam na Ruvu Shooting iliifunga 1-0 Mtibwa Sugar Uwanja wa Mabatini Mlandizi, Pwani.
    Stand United ililazimishwa sare ya 0-0 na Mbao FC Uwanja wa Kambarage Jumamosi Prisons ikashinda ugenini 1-0 dhidi ya Maji Maji Uwanja wa Maji Maji, Songea wakati Jumapil Mbeya City ililazimisha sare ya 0-0 na Kagera Sugar Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.
    Toto African ya Mwanza ilianza vyema Ligi Kuu baada ya kushinda bao 1-0 dhidi ya Mwadui FC ya Shinyanga, bao ekee, Waziri Junior dakika ya 36 aliyemshinda mbio beki wa Mwadui na kufumua shuti dhaifu lililomshinda kipa na kutinga nyavuni. 
    Huo unakuwa mwanzo mzuri kwa kocha Rogasian Kaijage aliyechukua nafasi iliyoachwa wazi, John Tegete aliyeondolewa baada ya msimu uliopita – na mwanzo mbaya wa kocha wa Mwadui, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’.
    Mechi za ufunguzi za Ligi Kuu Jumamosi, Simba SC iliichapa Ndanda FC 3-1 Uwanja wa Taifa, Azam ililazimishwa sare ya 1-1 na African Lyon Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam, Ruvu Shooting iliifunga 1-0 Mtibwa Sugar uwanja wa Mabatini Mlandizi, Pwani na Stand United ikalazimishwa sare ya 0-0 na Mbao FC Uwanja wa Kambarage Jumamosi Prisons ikashinda ugenini 1-0 dhidi ya Maji Maji Uwanja wa Maji Maji, Songea wakati Jumapil Mbeya City ililazimisha sare ya 0-0 na Kagera Sugar Uwanja wa Kambarage, Shinyanga kabla ya Toto kuilaza 1-0 Mwadui Jumatano Kirumba.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA KUENDELEZA UBABE LIGI KUU LEO? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top