• HABARI MPYA

    Thursday, August 25, 2016

    GUARDIOLA APANGWA NA BARCA, ARSENAL YAPEWA PSG MAKUNDI LIGI YA MABINGWA

    MAKUNDI YOTE LIGI YA MABINGWA ULAYA
    Kundi A; Arsenal PSG, Basle na Ludogorets
    Kundi B; Benfica, Napoli, Dynamo Kyiv na Besiktas
    Kundi C; Barcelona, Man City, Borussia Monchengladbach na Celtic
    Kundi D; Bayern Munich, Atletico Madrid, PSV Eindhoven na Rostov 
    Kundi E; CSKA Moscow, Bayer Leverkusen, Tottenham na 
    Monaco 
    Kundi F; Real Madrid, Borussia Dortmund, Sporting Lisbon na Legia Warsaw 
    Kundi G; Leicester, Porto, Club Bruges na Copenhagen 
    Kundi H; Juventus, Sevilla, Lyon na Dinamo Zagreb
    Kocha mpya wa Manchester City, Pep Guardiola amepangwa na timu yake ya zamani, Barcelona  PICHA ZAIDI GONGA HAPA

    KOCHA Pep Guardiola atakutana Barcelona baada ya timu yake mpya, Manchester City kupangwa kundi moja na timu yake hiyo ya zamani katika Ligi ya Mabingwa Ulaya. 
    Pep aliyetwaa taji hilo mara mbili akiwa na Barca, ameiwezesha City kuingia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa baada ya kuitoa Steaua Bucharest katika mchujo.
    Timu hizo mbili zimepangwa pamoja katika Kundi C dhidi ya Borussia Monchengladbach ya Ujerumani na mabingwa wa Scotland, Celtic. 
    Katika droo iliyopangwa leo, Arsenal imewekwa Kundi A pamoja na Paris Saint-Germain, Basle na Ludogorets wakati Kundi B kuna Benfica, Napoli, Dynamo Kyiv na Besiktas.
    Kundi D kuna Bayern Munich, Atletico Madrid, PSV Eindhoven na Rostov, Kundi E kuna CSKA Moscow, Bayer Leverkusen, Tottenham na Monaco, Kundi F kuna Real Madrid, Borussia Dortmund, Sporting Lisbon na Legia Warsaw. 
    Kundi G kjuna Leicester City, Porto, Club Bruges na Copenhagen, Kundi H kuna Juventus, Sevilla, Lyon na Dinamo Zagreb.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: GUARDIOLA APANGWA NA BARCA, ARSENAL YAPEWA PSG MAKUNDI LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top