• HABARI MPYA

    Tuesday, August 30, 2016

    DAR MUSICA KUZINDULIWA RASMI SEPTEMBA 16

    Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    BENDI ya Dar Music inatafanya uzinduzi wake rasmi Septemba 16, kwenye Ukumbi wa Mango Gardeni, jijini Dar es Salaam, ambao utasindikizwa na  Malkia wa mipasho nchini Khadij Kopa pamoja na bendi ya Msondo.
    Uzinduzi huo utaenda sambamba na utambulisho wa albamu ya bendi hiyo iliyobeba nyimbo 6 pamoja na video ya wimbo wao wa Chozi la Maskini.
    Akizungumza Jijini Dar es Salaam leo Meneja wa bendi hiyo Khamis Maero alisema kuwa uzinduzi huo mkubwa unafanyika kwa mara ya kwanza toka rais mpya Jado Fideforce aingie madarakani.
    Kiongozi wa Bendi ya Dar Musica,  Edward Anthony 'Fide Force' akizungumzia uzinduzi rasmi wa nendi yao, unaotarajia kufanyika Septemba 16, kwenye Ukumbi wa Mango Garden ulipo Kinondoni Dar es Salaam, wa kwanza kulia ni Meneja wa bendi hiyo Hamis Maero  

    Alisema kuwa utambulisho huo pia utatumika kwa ajili ya kutambulisha wanamuziki wapya waliojinga na bendi hiyo.
    Naye Kiongozi wa bendi hiyo Edward Anthony 'Fide Force' alisema kuwa nyimbo zitakazotmbulishwa katika uzinduzi huo ni pamoja na wimbo uliobeba albamu yao ya Chozi la Maskini pamoja na Salmaga.
    Nyimbo nyingine ni Bongo mchango, Maisha Upendo, Mtu Box, Jibebishe  na Ama zao Ama zangu.
    Alisema ndani ya bendi yake ameamua kuchukua wanamuziki wazuri ili kuifanya kuwa bora zaidi.
    "Ndani ya bendi yangu nimeamu kuchukua wanamuziki wazuri ili kuhimili ushindani uliopo katika tasnia ya muziki kutokana na ushindani uliopo" alisema Fideforce.
    Alisema kuwa ana uzoefu mkubwa na kile kinachopelekea bendi nyingi kuvunjika hivyo hawawezi kuruhusu kitu hicho kitokee ndani ya bendi yao.
    "Uzuri ni kwamba ninaelewa muziki wa bongo ulivyo na nini huwa kinafanyika na kipi cha kuepuka ili bendi kutovunjika" , alisema.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: DAR MUSICA KUZINDULIWA RASMI SEPTEMBA 16 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top