• HABARI MPYA

    Tuesday, August 09, 2016

    MO BEJAIA WAINGIA DAR KIMYA KIMYA, WAVAMIA KAMBI, UWANJA WA YANGA

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    TIMU ya Mouloudia Olympique Bejaia ya Algeria jioni ya leo imefanya mazoezi kwenye Uwanja wa Boko Veterani, Dar es Salaam kujiandaa na mchezo dhidi ya wenyeji, Yanga mwishoni mwa wiki.
    Yanga watawakaribisha Mouloudia Olympique Bejaia Jumamosi katika mchezo wa marudiano Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Na timu hiyo ya Algeria imefikia kwenye hoteli ya Ledger Plaza, Kunduchi, Dar es Salaam, ambayo mara kadhaa wenyeji wao, Yanga huweka kambi na kufanya pia mazoezi Uwanja wa Boko.
    Wachezaji wa Mouloudia Olympique Bejaia ya Algeria wafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Boko Veterani, Dar es Salaam leo
    Mouloudia Olympique Bejaia watamenyana na Yanga Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

    Yanga bado haijaingia kambini na inafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Gymkhana, katikati ya Jiji tangu wiki iliyopita kujiandaa na mchezo huo.
    Yanga itaingia katika mchezo wa jumamosi ikitoka kucheza mechi tano bila kushinda ikilazimishwa sare ya 0-0 na Mtibwa Sugar ya Morogoro katika mchezo wa kirafiki, ikifungwa 1-0 mara mbili, na Mouloudia Olympique Bejaia nchini Algeria na TP Mazembe Dar es Salaam kabla ya kutoa sare ya 1-1 na Medeama SC mjini hapa na baadaye kwenda kufungwa 3-1 na timu hiyo nchini Ghana katika mchezo wa marudiano.
    Mara ya mwisho Yanga kushinda ilikuwa ni kwenye Fainali ya Kombe la TFF, ilipoibugiza Azam FC 3-1 Uwanja wa Taifa. 
    Yanga itahitimisha mechi zake za Kundi A Kombe la Shirikisho kwa kumenyana na wenyeji TP Mazembe ya DRC mjini Lubumbashi Agosti 23, mwaka huu.
    Mazembe inaongoza Kundi A kwa pointi zake 10 baada ya mechi nne, ikishinda tatu na kutoa sare moja, ikifuatiwa na Bejaia na Medeama, ambazo kila moja ina pointi tano za sare tatu na ushindi mmoja, wakati Yanga inashika mkia kwa pointi yake moja. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MO BEJAIA WAINGIA DAR KIMYA KIMYA, WAVAMIA KAMBI, UWANJA WA YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top