• HABARI MPYA

  Friday, August 19, 2016

  KUNRADHI;

  MAPEMA leo tulipandisha habari yenye kichwa kisemacho; "KESSY ATAKIWA KUILIPA SIMBA MILIONI 120 AANZE KUCHEZEA YANGA WAKATI WOWOTE.
  Habari hiyo ilikuwa ina mapungufu na kwa ujumla haikuwa sahihi, ingawa haikuwa mbali sana na ukweli. Kwa dhati BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE tunakiri kosa juu ya habari hiyo, kwani tuliandika tofauti na tulivyopaswa kuandika – kulingana na maelezo ya chanzo cha habari yenyewe.
  Habari yenyewe kwa usahihi ilifuatia baadaye na tukaipandisha chini ya kichwa kisemacho; TAARIFA RASMI YA TFF KUHUSU HASSAN KESSY NA MKATABA WA SIMBA 
  Tunachukua fursa hii kuwaombaa radhi wasomaji wetu, hususan waathirika wa moja kwa moja na makosa haya – klabu ya Yanga na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). Pamoja na hayo, tunaahidi kuongeza umakini katika uchukuaji, uandikaji na upandishaji wa habari, ili kuepuka makosa kama haya. Asanteni.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KUNRADHI; Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top