• HABARI MPYA

  Friday, August 19, 2016

  MARTIN JOL ABWAGA MANYANGA AL AHLY, OSSAMA APEWA TIMU

  KOCHA Mholanzi, Martin Jol ameondoka klabu ya Al Ahly ya Misri baada ya matokeo mabaya kwa Mashetani hao Wekundu kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi mwaka huu.
  Kocha huyo alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya sare ya 2-2 nyumbani dhidi ya Zesco United ya Zambia mjini Suez ambayo yalizima ndoto za Ahly’ kutwaa taji la tisa la michuano hiyo. 
  Mkongwe Emad Meteab aliwanusuru mabingwa wa Misri kufungwa nayumbani kwa bao la kusawazisha la dakika za lala salama.
  “Bodi ya Wakurugenzi ya Ahly imekubaliana na Martin Jol kusitisha Mkataba katika mazingira ya kawaida na kwa heshima. Imeamuliwa Msaidizi wake, Ossama Orabi ataiongoza timu katika mchezo ujao dhidi ya ASEC Mimosas mjini Abidjan,”imesema taarifa katika tovuti ya klabu.
  Ahly itasafari kwenda Abidjan Jumatano ijayo (Agosti 24 mwaka 2016) kumenyana na ASEC katika mchezo wa Kundi A kukamilisha ratiba baada ya kupoteza nafasi ya kwenda Nusu Fainali.
  Jol aliteuliwa kuwa kocha wa Ahly miezi sita iliyopita na akawawezesha Mashetani Wekundu kutwaa ubingwa wa Ligi ya Misri wakiwapiku mahasimu wao, Zamalek. 
  Hata hivyo akafungwa mabao 3-1 na Zamalek katika fainali ya Kombe la Misri kabla ya sare ya 2-2 na Zesco na kuzima ndoto za Mashetani hao Wekundu kutwaa mataji matatu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MARTIN JOL ABWAGA MANYANGA AL AHLY, OSSAMA APEWA TIMU Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top