• HABARI MPYA

  Friday, August 19, 2016

  GWIJI WA MUZIKI WA TAARAB, BI SHAKILA SAID AAGA DUNIA

  MWIMBAJI mkongwe wa taarab aliyeitikisa Afrika Mashariki kwa sauti yake tamu, Bi Shakila Said amefariki dunia usiku huu. 
  Kwa mujibu wa www.saluti5.com mtoto wa marehemju aitwaye Shani amesema kwamba Bi Shakila amefariki baada ya kudondoka ghafla. 
  “Mama hakuwa mgonjwa hata kidogo, aliswali swala ya magharibi vizuri na baadae kidogo akadondoka na kufariki,” alisema Shani huku akilia. 
  Bi Shakila amefia nyumbani kwake Charambe jijini Dar es Salaam na mwili wake tayari umepelekwa kuhifadhiwa katika hospitali ya Temeke. 
  Kwa mujibu wa Shani, kwa sasa hivi bado hakuna utaratibu wowote wa mazishi uliopangwa. 
  Katika uhai wake Shakila alitamba zaidi katika vikundi vya Luck Star na Black Star za Tanga pamoja na JKT Taarab ya Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GWIJI WA MUZIKI WA TAARAB, BI SHAKILA SAID AAGA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top