• HABARI MPYA

  Sunday, August 07, 2016

  KIINGILIO RAHISI SIMBA DAY KESHO BUKU TANO TU TAIFA

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  KIINGILIO cha chini katika mchezo wa kirafiki baina ya wenyeji Simba SC na AFC Leopards ya Kenya Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kitakuwa ni Sh. 5,000.

  Taarifa ya Ofisa Habari wa Simba SC, Hajji Sunday Manara 'Zungu' kwa vyombo vya Habari leo, imesema kwamba viingilio vingine kwenye mechi hiyo ni Sh 10,000 kwa viti vya Orange Sh 15, 000 kwa VIP C, Sh. 20,000 kwa VIP B na Sh 25, 000 kwa VIP A.
  Manara amesema maandalizi yote yamekamilika na mchezo huo utakaokwenda na sherehe za miaka 80 ya Simba SC, maarufu kama Simba Day, utatanguliwa na burudani mbalimbali, ikiwemo bendi ya African Stars 'Twanga Pepeta'.
  Frederick Blagnon ataichezea Simba katika mechi ya kwanza Uwanja wa Taifa kesho
  "Mbali ya burudani hizo, pia kutakuwa na shamrashamra nyingine, zitakazonegesha kilele cha wiki ya sherehe zetu, zinazojulikana kwa umaarufu wa Simba Day. Klabu pia itatumia mechi ya kesho kuwatambulisha wachezaji wote watakaotumika kwenye msimu ujao wa ligi 2016|17 wakiwemo wale wapya waliosajiliwa msimu huu,"imesema taarifa ya Manara.
  Katika sherehe za kesho, Manara amesema Simba pia itazindua rasmi jezi mpya za msimu, ambazo zitaanza kuuzwa uwanjani kwa Sh 20,000 kila moja.
  Amesema Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ataongoza viongozi mbali mbali wa kitaifa kwenye sherehe hizo muhimu ambazo pia ni maadhimisho ya miaka themanini toka kuanzishwa kwa klabu yetu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIINGILIO RAHISI SIMBA DAY KESHO BUKU TANO TU TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top