• HABARI MPYA

  Friday, January 08, 2016

  YANGA SC NA MTIBWA SUGAR KATIKA PICHA JANA UWANJA WA AMAAN

  Kipa wa Mtibwa Sugar, Said Mohammed, akiruka bila mafanikio kuzuia shuti la mpira wa adhabu la mshambuliaji wa Yanga SC, Issoufou Boubacar (hayupo pichani) lililotinga nyavuni katika mchezo wa Kundi B Kombe la Mapinduzi usiku wa jana Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Yanga SC ilishinda 2-1 na kutinga Fainali kama kinara wa kundi, ikifuatiwa na Mtibwa.
  Kiungo wa Yanga SC, Thabani Kamusoko akimuacha chini mchezaji wa Mtibwa Sugar
  Mshambuliaji wa Yanga SC, Donald Ngoma akimiliki mpira mbele ya beki wa Mtibwa Sugar, Salim Mbonde. Kulia ni beki mwingine wa Mtibwa, Issa Rashid 'Baba Ubaya'
  Beki wa Yanga SC, Juma Abdul (kushoto) akiruka juu kupiga mpira kichwa dhidi ya Muzamil Yassin wa Mtibwa Sugar
  Mshambuliaji wa Yanga SC, Paul Nonga akimiliki mpira katikati ya mabeki wa Mtibwa Sugar, Dickson Daud (kulia) na Issa Rashid (kushoto)
  Mfungaji wa bao la ushindi la Yanga SC, Malimi Busungu (kushoto) akimtoka Issa Rashid wa Mtibwa
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC NA MTIBWA SUGAR KATIKA PICHA JANA UWANJA WA AMAAN Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top