MABINGWA watetezi, Yanga SC wamefanikiwa kwenda Fainali ya Kombe la Muungano baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Azam FC usiku hui Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
Mabao ya Yanga SC yamefungwa na mshambuliaji Mzimbabwe, Prince Mpumelelo Dube dakika ya tisa akiiadhibu timu yake ya zamani na kiungo Mkongo, Maxi Mpia Nzengeli dakika ya 25, wakati bao pekee la Azam FC limefungwa na kiungo mzawa, Feisal Salum Abdallah dakika ya 78 akiiadhibu timu yake ya zamani.
Yanga sasa itakutana na mshindi wa Nusu Fainali ya pili kati ya Simba SC na Mlandege FC kesho zitakazomenyana kuanzia Saa 2:15 usiku hapo hapo Uwanja wa Amaan.
Fainali ya Kombe la Muungano 2026 itapigwa Jumatano, Aprili 29 kuanzia Saa 2:15 usiku hapo hapo New Amaan Complex.


.png)
0 comments:
Post a Comment