TIMU ya Azam FC imefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Kombe la Muungano baada ya us Hindi wa mabao 2-0 dhidi ya KVZ FC usiku huu Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
Mabao yote ya Azam FC yamefungwa na mshambuliaji wa Kimataifa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Jean-Jacques Ngita Kamanga dakika ya 40 na 54.
Azam FC sasa itakutana na bingwa mtetezi, Yanga katika Nusu Fainali ya michuano hiyo Jumamosi kuanzia Saa 2:15 usiku hapo hapo Uwanja wa New Amaan Complex.
Hatua ya Robo Fainali ya michuano hiyo itakamilishwa kesho kwa mechi mbili, Singida Black Stars kumenyana na Mlandege FC kuanzia Saa 10:15 jioni na Simba SC dhidi ya Mafunzo FC kuanzia Saa 2:15 usiku hapo hapo Uwanja Amaan.
Ikumbukwe Yanga ililuwa ya kwanza kutinga Nusu Fainali kwa kuitoa Muembe Makumbi City kwa kuichapa 4-0 jana hapo hapo New Amaan Complex.
Nusu Fainali ya pili itafuatia Aprili 26 na Fainali ya Muungano Cup 2026 itapigwa Aprili 29 mechi zote zikichezwa Uwanja wa New Alana Complex, Zanzibar.



.png)
0 comments:
Post a Comment