• HABARI MPYA

  Tuesday, January 05, 2016

  SIMBA SC YAKABWA KOO, SARE 2-2 NA WAPEMBA

  MAKUNDI, MATOKEO NA RATIBA KOMBE LA MAPINDUZI 2016
  Kundi A: Simba SC, Jamhuri, JKU, URA
  Kundi B: Yanga SC, Mafunzo, Azam FC, Mtibwa Sugar
  (Mechi zote zitachezwa Uwanja wa Amaan, Zanzibar)

  Jan 3, 2016
  Yanga SC 3-0 Mafunzo
  Mtibwa Sugar 1-1 Azam FC (Saa 2:15 usiku)
  Jan 4, 2016
  JKU 1-3 URA (Saa 10:15 jioni)
  Simba SC 2-2 Jamhuri Saa 2:15 usiku)
  Jan 5, 2016
  Mafunzo Vs Mtibwa Sugar (Saa 10:15 jioni)
  Azam FC Vs Yanga SC (Saa 2:15 usiku)
  Jan 6, 2016
  Jamhuri Vs JKU (Saa 10:15 jioni)
  URA Vs Simba SC (Saa 2:15 usiku)
  Jan 7, 2016
  Azam Vs Mafunzo (Saa 10:15 jioni)
  Mtibwa Sugar Vs Yanga (Saa 2:15 usiku)
  Jan 8, 2016
  Jamhuri Vs URA (Saa 10:15 jioni)
  Simba SC Vs JKU (Saa 2:15 usiku)
  NUSU FAINALI
  Jan 10, 2016
  FAINALI
  Jan 13, 2016 (Saa 2:15 usiku)
  Awadh Juma akishangilia baada ya kuifungia bao la kusawazisha Simba SC

  MABINGWA watetezi, Simba SC wameanza kwa sare ya 2-2 na Jamhuri ya Pemba katika mchezo wa Kundi A, Kombe la Mapinduzi usiku wa Jumatatu Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
  Matokeo hayo yanaiweka Simba SC katika nafasi ngumu kidogo kusonga Nusu Fainali ya michuano hiyo, kufuatia URA ya Uganda kuanza na ushindi wa 3-1 dhidi ya JKU ya Zanzibar katika mchezo uliotangulia siku hiyo.
  Mabao ya Simba SC yamefungwa na kiungo Mzanzibari, Awadh Juma Issa moja kila kipindi, wakati ya Jamhuri yamefungwa na Mwalim Mohammed na Ammy Khamis.
  Awadh alianza kuwafungia Simba SC dakika ya 12, baada ya kuwatoka mabeki wa Jamhuri na kuachia shuti la mbali lililomshinda kipa na kuingia moja kwa moja nyavuni.
  Mwalim Mohammed akawasawazishia wababe wa Pemba dakika ya 15, baada ya kuwatoka mabeki wa Simba na kupiga shuti lilomshinda kipa Peter Manyika.
  Ammy Mohammed akaifungia bao la pili Jamhuri dakika ya 53 kabla ya Awadh Juma kuifungia Simba SC bao la pili la kusawazisha baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa JKU.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAKABWA KOO, SARE 2-2 NA WAPEMBA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top