• HABARI MPYA

  Monday, January 04, 2016

  BENITEZ AKALIA KUTI KAVU REAL MADRID, ZIDANE KUPEWA NAFASI YAKE

  KOCHA Rafa Benitez yuko kwenye hatari ya kufukuzwa kiasi cha miezi saba tu tangu achukue nafasi Real Madrid.
  Wakurugenzi wa klabu hiyo ya Hispania wamekuwa katika mikakati Jumatatu yote baada ya timu hiyo kushindwa kuifunga Valencia jioni ya Jumapili katika La Liga.
  Rais wa klabu, Florentino Perez ameitisha kikao cha bodi Jumatatu mchana ambacho kinatarajiwa kufuatiwa na Mkutano na Waandishi wa Habari baadaye.

  Rafa Benitez anatarajiwa kufukuzwa na nafasi yake kuchukuliwa na gwiji wa klabu, Zinedine Zidane


  Matarajio ni kwamba, Benitez atafukuzwa na gwiji wa klabu, Zinedine Zidane atapandishwa kutoka timu B awe kocha wa timu A hadi mwishoni mwa msimu.
  Perez anafahamika kuwa shabiki mkubwa wa kocha Mreno, Jose Mourinho ambaye pia ni kocha wa zamani wa Chelsea, ambaye anapewa nafasi kubwa ya kurejea Santiago Bernabeu.
  Kwa hakika, Mourinho anapewa nafasi kubwa ya kurejea kwa vigogo hao wa Hispania mwishoni mwa msimu iwapo Zidane hatafanya vizuri.
  Benitez hajashinda mchezo wowote mkubwa wa ugenini wa Madrid msimu huu wakifungwa na Villarreal, Sevilla na Barcelona huku pia wakiachia pointi kwa Atletico Madrid, Valencia na Paris Saint-Germain.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BENITEZ AKALIA KUTI KAVU REAL MADRID, ZIDANE KUPEWA NAFASI YAKE Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top