• HABARI MPYA

  Monday, January 11, 2016

  SIMBA SC NA MTIBWA SUGAR KATIKA PICHA ZANZIBAR JANA

  Kiungo wa Mtibwa Sugar, Mohammed Ibrahim (katikati) akipasua katikati ya wachezaji wa Simba SC, Emery Nimubona (kulia) na Danny Lyanga (kushoto) katika Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi jana jioni Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Mtibwa ilishinda 1-0 na sasa itakutana na URA katika fainali Jumatano
  Kiungo wa Simba SC, Justice Majabvi akipasua katikati ya wachezaji wa Mtibwa Sugar, Shaaban Nditi (kulia) na Salim Mbonde (kushoto) jana
  Mshambuliaji wa Simba SC, Ibrahim Hajib (kushoto) akimtoka bekii wa Mtibwa, Salim Mbonde
  Kiungo wa Simba SC, Mwinyi Kazimoto akiwatoka wachezaji wa Mtibwa Sugar kabla ya kukosa bao la wazi jana
  Kiungo wa Simba SC, Jonas Mkude akimiliki mpira mbele ya kiungo wa Mtibwa, Shaaban Nditi jana
  Beki wa Mtibwa Sugar, Ally Shomary akimtoka beki wa Simba SC, Mohammed Hussein 'Tshabalala'
  Mshambuliaji wa Simba SC, Mussa Mgosi (kulia) akimtoka beki wa Mtibwa Sugar, Dickson Daud (kushoto)
  Danny Lyanga wa Simba SC na Dickson Daud wa Mtibwa Sugar wakiwania mpira wa juu jana
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC NA MTIBWA SUGAR KATIKA PICHA ZANZIBAR JANA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top