• HABARI MPYA

  Saturday, January 16, 2016

  NYIGU WAUA TEMBO, RWANDA WAILAZA 1-0 IVORY COAST UFUNGUZI CHAN 2016

  WENYEJI Rwanda wameanza vyema Michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) baada ya kuichapa bao 1-0 jioni ya leo Uwanja wa Amahoro, Kigali.
  Shukrani kwake mfungaji wa bao hilo pekee, beki Emery Bayisenge (pichani kulia) aliyewainua vitini mashabiki wa Amavubi dakika ya 60 kwa shuti la mpira wa adhabu.
  Katika mchezo huo uliohudhuriwa na Rais wa Rwanda, Paul Kagame Amavubi, yaani Nyigu walicheza vizuri hususan kipindi cha kwanza na kuwapoteza kabisa wageni.
  Rwanda sasa inaanzia kileleni mwa Kundi A kwa pointi zake tatu, wakati mchezo wa pili wa kundi hilo baina ya Gabon na Morocco unafuatia sasa kwenye Uwanja huo huo.
  Michuano hiyo inayohusisha wachezaji wanaocheza Ligi za nchini mwao pekee itaendelea kesho kwa mechi za Kundi B, mabingwa wa kwanza wa michuano hiyo, DRC wakimenyana na Ethiopia Uwanja wa Huye kuanzia Saa 10:00 jioni, kabla ya Angola kumenyana na Cameroon Uwanja wa Huye pia kuanzia Saa 1:00 usiku.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NYIGU WAUA TEMBO, RWANDA WAILAZA 1-0 IVORY COAST UFUNGUZI CHAN 2016 Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top