• HABARI MPYA

    Sunday, March 22, 2026

    ESPERANCE WAITUPA NJE AL AHLY LIGI YA MABINGWA AFRIKA

    TIMU ya Espérance ya Tunisia imefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya wenyeji, Al Ahly SC katika mchezo wa marudiano wa Robo Fainali usiku wa Jumamosi Uwanja wa Cairo International Jijini Cairo.
    Mabao ya Esperance yamefungwa na mshambuliaji Mfaransa mwenye asili ya Ivory Coast, Florian Thomas Danho Séké dakika ya 68‎ na mabeki, Mohamed Amine Tougai dakika ya 78 na Hamza Jelassi dakika ya 90’‎+‎4‎.
    Kwa upande wao mabingwa wa Kihistoria Afrika, Al Ahly mabao yao yamefungwa na mshambuliaji Mahmoud Hassan ‘Trezeguet’ dakika ya 10 na Hamza Jelassi aliyejifunga dakika ya 84..
    Kwa matokeo hayo, Espérance inakwenda Nusu Fainali kwa ushindi wa jumla wa 4-2 kufuatia kushinda 1-0 kwenye mchezo wa kwanza Machi 16 bao la mkwaju wa penalti wa beki wa kati, Mohamed Amine Tougai dakika ya 73 Uwanja wa Olimpiki Hammadi-Agrebi, Radès, Kusini mwa Jiji la Tunis – mchezo ambao Al Ahly walimlalamikia mno refa Msenegal, Issa Sy. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ESPERANCE WAITUPA NJE AL AHLY LIGI YA MABINGWA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top