• HABARI MPYA

  Saturday, January 16, 2016

  CHELSEA BADO ‘UGONJWA WA MOYO’, YATOA SARE 3-3 NA EVERTON DARAJANI, MAN CITY YAWATANDIKA PALACE 4-0 LIGI KUU ENGLAND

  MATOKEO LIGI KUU YA ENGLAND LEO
  Januari 16, 2016  
  Manchester City 4-0 Crystal Palace
  Newcastle United 2-1 West Ham United
  Southampton 3-0 West Bromwich Albion
  Chelsea 3-3 Everton
  Bournemouth 3-0 Norwich City
  Tottenham Hotspur 4-1 Sunderland
  Aston Villa Vs Leicester (Inaendelea)
  Kesho; Januari 17, 2016
  Liverpool Vs Manchester United (Saa 11:05 jioni)
  Stoke City Vs Arsenal (Saa 1:15 usiku)

  Nahodha wa Chelsea, John Terry akishangilia na mashabiki wa Chelsea baada ya kufunga bao la kusawazisha dhidi ya Everton Uwanja wa Stamford Bridge leo PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  HAMKANI bado si shwari Chelsea, baada ya usiku wa leo kulazimishwa sare ya kufungana mabao 3-3 na Everton katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Stamford Bridge, London.
  Nahodha John Terry aliinusuru timu yake baada ya kufunga bao la kusawazisha dakika ya 98, kufuatia Everton kuongoza kwa mabao 3-2 tangu dakika ya 90.
  Bao hilo la Terry lilipoza hasira za mashabiki wa The Bluse dhidi yake kutokana na kujifunga dakika ya 50 kuwapatia bao la kwanza Everton.
  Mabao mengine ya Everton yalifungwa na Kevin Mirallas dakika ya 56 na Ramiro Funes Mori dakika ya 90, wakati mabao mengine ya Chelsea yamefungwa na Diego Costa dakika ya 64 na Cesc Fabregas dakika ya 66.

  Mshambuliaji wa Manchester City, Sergio Aguero (kushoto) akishangilia na Kelechi Iheanacho baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Crsytal palace Uwanja wa Etihad leo  PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Manchester City wamepata ushindi mnono wa 4-0 dhidi ya Crystal Palace, mabao ya Fabian Delph dakika ya 22, Sergio Aguero mawili dakika ya 41 na 68 na David Silva dakika ya 84 Uwanja wa Etihad.
  Newcastle United imeshinda 2-1 dhidi ya West Ham United, mabao yake yakifungwa na Ayoze Perez Gutierrez dakika ya sita na Georginio Wijnaldum dakika ya 15, huku la wageni likifungwa na Nikica Jelavic dakika ya 49 Uwanja wa St. James' Park.
  Southampton imeshinda 3-0 nyumbani dhidi ya West Bromwich Albion, mabao ya James Ward-Prowse dakika ya tano na 35 kwa penalti na Dusan Tadic dakika ya 72 Uwanja wa St. Mary's.
  Bournemouth pia imeshinda 3-0 nyumbani dhidi ya Norwich City, mabao ya Dan Gosling dakika ya 10, Charlie Daniels kwa penalti dakika ya 54 na Benik Afobe dakika ya 75 Uwanja wa Vitality.
  Tottenham Hotspur imeshinda 4-1 dhidi ya Sunderland, Christian Eriksen akifunga mabao mawili dakika ya 42 na 67, huku mengine yakifungwa na Mousa Dembele dakika ya 59 na Harry Kane kwa penalti dakika ya 79, huku bao la wageni likifungwa na Patrick van Aanholt dakika ya 40 Uwanja wa White Hart Lane.
  Mechi kati ya Aston Villa na Leicester City inaendelea hivi sasa Uwanja wa Villa Park timu hizo zikiwa hazijafungana.
  Ligi Kuu ya England itaendelea kesho kwa mechi mbili, Liverpool na Manchester United Uwanja wa Anfield kuanzia Saa 11:05 na Stoke City na Arsenal Uwanja wa Britannia kuanzia Saa 1:15 usiku.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHELSEA BADO ‘UGONJWA WA MOYO’, YATOA SARE 3-3 NA EVERTON DARAJANI, MAN CITY YAWATANDIKA PALACE 4-0 LIGI KUU ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top