• HABARI MPYA

    Thursday, March 19, 2026

    SIMBA SC YATOA SARE NA PAMBA, 1-1 KIRUMBA

    TIMU ya Simba SC imetoa sare ya kufungana bao 1-1 na wenyeji, Pamba Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza. 
    Ni Simba SC waliotangulia kwa bao la winga wa kushoto Muivory Coast, Alain Anicet Oura dakika ya 33, kabla ya mshambuliaji James Mwashinga kuisawazishia Pamba dakika tatu baadaye.
    Kwa matokeo hayo, Simba SC inafikisha pointi 27 katika mechi ya 13 na kuendelea kubaki nafasi ya nne na Pamba Jiji FC inafikisha pointi 25 katika mechi ya 26, nayo inabaki nafasi ya tano.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC YATOA SARE NA PAMBA, 1-1 KIRUMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top