• HABARI MPYA

  Sunday, January 17, 2016

  NGASSA AIONGOZA FREE STATE KUSHINDA 2-1 UGENINI LIGI KUU YA AFRIKA KUSINI

  NYOTA wa Tanzania, Mrisho Khalfan Ngassa (pichani juu) ameiongoza timu yake, Free State Stars kupata ushindi wa ugenini wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji Platinum Stars katika Ligi Kuu ya Afrika Kusini.
  Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Moruleng, Ngassa – mchezaji wa zamani wa Azam, Simba na Yanga alicheza kwa dakika 76 kabla ya kumpisha Fileccia.
  Na Ngassa alikuwa mwiba kwa safu ya ulinzi ya Platinum Stars na akakaribia kufunga mwenyewe dakika ya 26 kama si shuti lake kuokolewa na kipa Mzimela.
  Mshambuliaji wa zamani wa Orlando Pirates, Ndumiso Mabena alianza kuifungia Platinum dakika ya 43 kabla ya Nahodha wa Ea Lla Koto, Paulus Masehe kuisawazishia timu yake dakika ya 51.
  Free State Stars walipewa penalti dakika ya 75, wakati Moeketsi Sekola alipoangushwa kwenye boksi na mfungaji bora wa Ligi Kuu ya ABSA msimu uliopita, Moeketsi Sekola akafunga dakika ya 79 kuipatia timu yake ushindi.
  Kikosi cha Platinum Stars kilikuwa; Mzimela, Semenya, Nhlapo, Gumede, Zulu, Mathe, Madondo/Ng'ambi dk59, Zongo/Segolela dk86, Msomi, Mabena na Ntuli/Madubanya dk74.
  Free State: Diakite, Masehe, Mashego, Sankara, Thlone, Chabalala, Nkausu, Sekola, Mohomi/Makhaula dk87, Ngassa/Fileccia dk76 na Jaftha/Kerspuy dk59.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NGASSA AIONGOZA FREE STATE KUSHINDA 2-1 UGENINI LIGI KUU YA AFRIKA KUSINI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top