• HABARI MPYA

  Monday, January 04, 2016

  MTIBWA SUGAR NA AZAM FC ZAGAWANA POINTI

  TIMU za Mtibwa Sugar na Azam FC zimegawana pointi katika mchezo wa Kundi B Kombe la Mapinduzi usiku wa Jumapili Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
  Matokeo hayo yanazifanya timu hizo za Tanzania Bara zifungane kwa kila kitu nyuma ya Yanga SC yenye pointi tatu na mabao matatu, wakati Mafunzo inashika mkia ikiwa haina pointi.
  Mtibwa Sugar walianza kupata bao kupitia kwa mshambuliaji Hussein Javu anayecheza kwa mkopo kutoka Yanga SC kabla ya Azam FC kusawazisha kupitia kwa Nahodha wake, John Bocco kwa penalti, ambaye yeye mwenyewe alichezewa rafu ndani ya boksi.

  Katika mchezo wa kwanza wa Kundi Jumapili Yanga SC iliichapa Mafunzo FC mabao 3-0 Uwanja wa Amaan.
  Mshambuliaji Mzimbabwe Donald Dombo Ngoma alifunga mabao mawili kipindi cha kwanza na mshambuliaji mpya, Paul Nonga akaingia mwishoni mwa kipindi cha pili na kufunga bao katika mpira wa kwanza kugusa.
  Mechi za Kundi A zinafuatia Jumatatu, JKU ikimenyana na URA Saa 10:15 jioni kabla ya Simba SC, mabingwa watetezi kumenyana na Jamhuri Saa 2:15 usiku.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR NA AZAM FC ZAGAWANA POINTI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top