• HABARI MPYA

  Saturday, January 16, 2016

  KIIZA ‘DIEGO’ AING’ARISHA SIMBA SC, YAILAZA MTIBWA 1-0 TAIFA, SASA YAIPUMULIA YANGA

  RATIBA LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA;
  Januari 16, 2016
  Simba SC 1-0 Mtibwa Sugar
  JKT Ruvu 1-5 Mgambo JKT
  Toto Africans 0-1 Prisons
  Stand United 1-0 Kagera Sugar
  Mbeya City 1-0 Mwadui FC
  Coastal Union 1-1 Majimaji
  Azam FC Vs African Sports (Saa 1:00 usiku)
  Januari 17, 2016
  Yanga SC Vs Ndanda FC

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  BAO pekee la mshambuliaji Hamisi Friday Kiiza ‘Diego’ limeipa Simba SC ushindi wa 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uganda, Kiiza aliifungia Simba SC bao hilo dakika ya tano tu kwa kichwa akimalizia krosi nzuri ya Ibrahim Hajib kutoka upande wa kushoto.
  Na sasa Simba SC inafikisha pointi 30 baada ya kucheza mechi 14, ikiendelea kukaa nafasi ya tatu nyuma ya mabingwa watetezi, Yanga SC pointi 32 za mechi 13 na vinara, Azam FC pointi 35 za mechi 13 pia.
  Azam FC watacheza mechi yao ya 14 usiku wa leo dhidi ya African Sports ya Tanga Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam, wakati Yanga SC watakuwa wenyeji wa Ndanda Uwanja wa Taifa kesho.
  Wachezaji wa Simba SC wakimpongeza Hamisi Kiiza (kushoto) baada ya kufunga leo Uwanja wa Taifa

  Pamoja na kufungwa, Mtibwa Sugar walionyesha upinzani kwa Simba SC na dakika ya 11, kiungo Shiza Kichuya alipoteza nafasi ya wazi baada ya shuti lake kuokolewa na kipa Vincent Angban, raia wa Ivory Coast.
  Dakika ya 44, Ally Shomari naye alipiga shuti kali, lakini kipa wa Simba SC, Vincent Angban akaokoa.
  Kizza naye alipoteza nafasi za kufunga dakika ya 15 na 33 baada ya kupiga nje.
  Kipindi cha pili, timu zote ziliendelea kushambuliana kwa zamani, lakini matokeo hayakubadilika. 
  Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Vincent Angban, Emery Nimubona, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Hassan Isihaka, Juuko Murshid, Justice Majabvi, Mwinyi Kazimoto, Jonas Mkude, Ibrahim Hajib/Danny Lyanga dk64, Hamisi Kiiza/Awadh Juma dk89 na Peter Mwalyanzi/Said Ndemla dk31.
  Mtibwa Sugar; Said Mohamed, Ally Shomary, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Salim Mbonde, Henry Joseph, Shaaban Nditi, Shiza Kichuya, Muzamil Yassin, Hussein Javu/Jaffar Kibaya dk64, Ibrahim Rajab ‘Jeba’ na Mohammed Ibrahim/Vincent Barnabas dk64.
  Mechi nyingine za Ligi Kuu leo; Prisons imeifunga Toto 1-0 Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, Stand United imeifunga 1-0 Kagera Sugar Uwanja wa Kambarage, Shinyanga, Mbeya City imeifunga 1-0 Mwadui FC Uwanja wa Sokoine, Mbeya na Coastal Union imelazimishwa sare ya 1-1 na Majimaji Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
  Mchezo kati ya vinara wa Ligi Kuu, Azam FC dhidi ya African Sports unafuatia sasa Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, wakati kesho mabingwa watetezi, Yanga wataikaribisha Ndanda FC ya Mtwara.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIIZA ‘DIEGO’ AING’ARISHA SIMBA SC, YAILAZA MTIBWA 1-0 TAIFA, SASA YAIPUMULIA YANGA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top