• HABARI MPYA

  Sunday, January 17, 2016

  DRC WAANZA NA MOTO CHAN 2016, WAITANDIKA ETHIOPIA 3-0 HUYE

  JAMHURI ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imeanza vyema michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) baada ya kuifunga Ethiopia mabao 3-0 katika mchezo wa Kundi B jioni ya Uwanja wa Huye mjini Kigali, Rwanda.
  Katika mechi hiyo ya tatu ya michuano hiyo inayoshirikisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee, DRC ilipata bao lake la kwanza kupitia kwa Guy Lusadisu dakika ya 44.
  Na baada tu ya kuanza kipindi cha pili, Heritier Luvumvu akaifungia DRC bao la pili dakika ya 46, kabla ya Meschack Elia kufunga la tatu dakika 10 baadaye.
  DRC imeanza vyema michuano ya CHAN 2016 kwa kuifunga Ethiopia 3-0

  Ushindi huo unawaweka kileleni DRC kabla ya mchezo mwingine wa kundi B, baina ya Angola na Cameroon.
  Mechi za ufunguzi za Kundi A jana, wenyeji Rwanda walishinda 1-0 dhidi ya Ivory Coast, bao pekee la beki Emery Bayisenge, wakati Gabon ilitoka sare ya 0-0 na Morocco.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DRC WAANZA NA MOTO CHAN 2016, WAITANDIKA ETHIOPIA 3-0 HUYE Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top