• HABARI MPYA

  Tuesday, September 30, 2014

  SARE ZAIKIMBIZA SIMBA SC ZANZIBAR, WAHAMISHIA KAMBI CHANGANYIKENI

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  BAADA ya kutoa sare mbili mfululizo katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simba SC imebadilisha kambi kutoka Zanzibar hadi Dar es Salaam.
  Simba SC iliingia kwenye mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu na Coastal Union ikitokea Zanzibar na baada ya sare 2-2 ikarejea tena visiwani humo.
  Lakini baada ya sare nyingine Jumamosi, 1-1 na Polisi Morogoro sasa vigogo hao wa soka ya Tanzania wameamua kubaki Dar es Salaam na leo kikosi kinaingia kambini hoteli ya Uplands, eneo la Changanyikeni.
  Miraj Adam kushoto ameanza mazoezi kujiandaa na mechi dhidi ya Stand United

  Habari njema zaidi ni kwamba mabeki wa pembeni Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ na Miraj Adam wameanza mazoezi leo Uwanja wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kujiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu.
  Simba SC itashuka dimbani Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kumenyana na Stand United ya Shinyanga kutafuta ushindi wa kwanza katika Ligi Kuu.
  Simba SC itaendelea kuwakosa kipa wake namba moja, Ivo Mapunda ambaye anatakiwa kuwa nje kwa wiki nane kwa maumivu ya kidole, beki Nassor Masoud Chollo anayeumwa enka na mshambuliaji Paul Kongera mwenye maumivu ya goti, yatakayomuweka nje kwa wiki sita.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SARE ZAIKIMBIZA SIMBA SC ZANZIBAR, WAHAMISHIA KAMBI CHANGANYIKENI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top