• HABARI MPYA

  Saturday, September 27, 2014

  MAN UNITED PUNGUFU YASHINDA 2-1...ROONEY ALIMWA NYEKUNDU KWA KUCHEZA RAFU

  MANCHESTER United imejitutumua na kupata ushindi mwembamba wa mabao 2-1 dhidi ya West Ham United Uwanja wa Old Trafford, licha ya kucheza pungufu baada ya Nahodha wake, Wayne Rooney kutolewa kwa kadi nyekundu.  
  Rooney alipewa kadi nyekundu ya moja kwa moja dakika ya 60 baada ya kumkwatua kwa nyuma kiungo wa West Ham, Stewart Downing.
  Lakini Rooney aliondoka uwanjani akiwa tayari ameifungia United bao lililokuwa la kwanza dakika ya tano, kabla ya Robin van Persie kufunga la pili dakika ya 23. 
  Wayne Rooney akishangilia baada ya kuifungia United bao la kwanza leo 

  Makosa ya kipa wa United, David De Gea yaliipa Hammers bao la kufutia machozi lililofungwa na Diafra Sakho dakika ya 37. Kevin Nolan aliifungia West Ham bao ambalo lingekuwa la kusawazisha dakika ya mwisho, lakini bahati alikuwa amekwishaotea.
  Kikosi cha Manchester United kilikuwa; De Gea, Rafael, McNair, Rojo, Shaw, Blind, Herrera/Valencia dk74, Di Maria/Thorpe dk90, Rooney, Van Persie na Falcao/Fletcher dk65.
  West Ham: Adrian, Demel/Jenkinson dk65, Tomkins, Reid, Cresswell, Song, Poyet, Amalfitano/Cole dk61, Downing, Sakho na E Valencia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED PUNGUFU YASHINDA 2-1...ROONEY ALIMWA NYEKUNDU KWA KUCHEZA RAFU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top