• HABARI MPYA

  Tuesday, September 30, 2014

  MALINDI YAONA MWEZI LIGI KUU ZENJI, YAILAZA 1-0 POLISI

  Na Ameir Khalid, DAR ES SALAAM
  BAADA kupoteza mechi mbili mfululizo katika Ligi Kuu ya soka Zanzibar Grand Malt, jana Malindi SC iliona mwezi baada ya kuitandika Polisi bao 1-0 uwanja wa Amaan.
  Katika mpambano huo ambao haukuhudhuriwa na watazamaji wengi,  Malindi ambayo kwenye michezo iliyopita ilionekana kucheza ovyo, jana waliimarika na kucheza mchezo wa maelewano kwa kupanga mashambulizi langoni mwa wapinzani wao.
  Nayo Polisi ambayo imepokea kipigo hicho cha kwanza siku moja tu baada ya kubarikiwa ushindi wa rufaa yake dhidi ya Hard Rock na kuzawadiwa mabao mawili na pointi tatu.
  Katika mchezo wake wa awalim timu hiyo ilitoka sare tasa na Hard Rock kabla kuishinda Shaba, michezo yote ikipigwa katika dimba la Gombani.

  Mshambuliaji wa Malindi Salum Masoud (jezi nyeupe) akitafuta mbinu ya kumpita beki wa Polisi katika mchezo wa ligi kuu Zanzibar uwanja wa Amaan Zanzibar.

  Bao la Malindi jana, lilipachikwa nyavuni na mchezaji Fakih Hijja katika dakika ya 16, baada ya kuunganisha mpira wa kona.
  Polisi walikuja juu na kuanza kupanga mashambulizi kwa lengo la kutaka kusawazisha, lakini washambuliaji wake walishindwa kutumia vyema nafasi nyingi walizopata.
  Kuanza kwa ngwe ya lala salama, Malindi walicheza zaidi kwa kupeleka mashambulizi langoni mwa Polisi lakini kama ilivyo kwa Polisi washambuliaji wake walishindwa kutumia vyema nafasi walizozipata.
  Uwanja wa Gombani Pemba, anaripoti kuwa timu za Hard Rock na Mtende zimetoka sare ya bao 1-1.
  Ligi hiyo itaendelea tena leo kwa mchezo kati ya KMKM na JKU uwanja wa Amaan, huku Shaba wakioneshana kazi na Mafunzo uwanja wa Gombani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MALINDI YAONA MWEZI LIGI KUU ZENJI, YAILAZA 1-0 POLISI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top