• HABARI MPYA

  Tuesday, September 23, 2014

  MAN UNITED YATAKIWA KUTUMIA PAUNI MILIONI 100 ZAIDI KUSAJILI BEKI LA KATI NA KIUNGO MKABAJI WA KIWANGO CHA DUNIA, USHAURI WA NEVILLE HUO

  BEKI wa zamani wa Manchester United, Phil Neville anaamini klabu hiyo inahitaji kutumia kiasi kingine cha Pauni Milioni 100 ili kuimarika kwa ushindani wa taji la Ligi Kuu ya England.
  Timu hiyo iliyomaliza katika nafasi ya saba msimu uliopita wa Ligi Kuu ya England, ilimuingiza sokoni kocha wake, Louis van Gaal kumwaga zaidi ya Pauni Milioni 150 kwa manunuzi ya Angel di Maria, Luke Shaw, Ander Herrera, Marcos Rojo, Daley Blind na Radamel Falcao aliyechukuliwa kwa mkopo.
  United iliyokwama kusajili beki wa kati, imejikuta kwenye tatizo la safu ya ulinzi msimu huu kutokana na Chris Smalling, Phil Jones na Jonny Evans ama kutokuwa vizuri kimchezo au kutokuwa fiti, wakati kinda Tyler Blackett anaangushwa na uzoefu licha ya kupewa majukumu.
  Vichwa vinawauma; Van  Gaal (katikati) na Wasaidizi wake wakati Manchester United ikicheza na Leicester Jumapili

  The Barclays Premier League table
  Msimamo wa Ligi Kuu England hadi sasa
  Na Neville anaamini hilo ni tatizo kubwa ambalo bado linahitaji ufumbuzi.
  "Nafahamu United imetumia Pauni Milioni 150,"amesema.
  "Nafikiri kuna uhamisho mwingine wa wachezaji wawili wa kiwango kile kile cha fedha unahitajika - labda Pauni Milioni 100- kabla hata hawajafikiria kushinda taji.
  "Bado kuna nafasi muhimu katika timu zinahitaji kujazwa. Nafikiri nafasi ya beki ya kati wazi ni muhimu. Kiungo mkabaji au kiungo wa kati anahitajika kuongezwa pia. Hakukuwa na mabeki wa kati wa kiwango cha dunia sokoni usajili wa msimu huu. Nafikiri hiyo ndiyo sababu katika madirisha mawili yajayo ya usajili, United itapaswa kutafuta beki wa kiwango cha kidunia,"amesema.
  Pamoja na hayo, amewataka mabeki wa England, Jones na Smalling kuhakikisha wanadhihirisha thamani yao katika klabu hiyo haraka iwezekanavyo. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED YATAKIWA KUTUMIA PAUNI MILIONI 100 ZAIDI KUSAJILI BEKI LA KATI NA KIUNGO MKABAJI WA KIWANGO CHA DUNIA, USHAURI WA NEVILLE HUO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top