• HABARI MPYA

  Saturday, September 27, 2014

  LIVERPOOL YALAZIMISHWA SARE NA EVERTON 1-1 ANFIELD

  LIVERPOOL imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Everton Uwanja wa Anfield, katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.
  Steven Gerrard alitangulia kufunga bao la kuongoza kwa Liverpool kwa shuti kali la mpira wa adhabu dakika ya 65, kabla ya Phil Jagielka kufunga la kusawazisha dakika ya 90.  
  Everton walilalamikia kunyimwa penalti wakati Alberto Moreno alipomuangusha kwenye eneo la hatari Romelu Lukaku na Liverpool walilalamika Gareth Barry aliunawa mpira kwenye eneo la hatari, lakini refa Martin Atkinson akapeta.
  Mario Balotelli wa Liverpool kulia alikosa bao la wazi akiwa amebaki na kipa Tim Howard
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YALAZIMISHWA SARE NA EVERTON 1-1 ANFIELD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top