• HABARI MPYA

  Monday, September 29, 2014

  KIPANGA YAITUNGUA CHUONI 2-0 AMAAN

  Na Ameir Khalid, ZANZIBAR
  TIMU ya Kipanga inayomilikiwa na JWTZ jana ilianza kuonja ladha ya ushindi baada ya kuitandika Chuoni  magoli 2-0, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Zanzibar,  mtanange uliopigwa uwanja wa Amaan.
  Huo ni ushindi wa kwanza kwa maafandi hao ambao wamepanda daraja msimu huu kufuatia kutoka sare kwenye mchezo  uliopita dhidi ya Miembeni na  kufungwa na Zimamoto.
  Hata hivyo, haikuwa rahisi  kwa maafandi hao kuweza kutoka na ushindi huo kwani hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika hakuna ambaye aliweza kutoka na ushindi licha ya kosa kosa nyingi kwa kila upande.

  Mshambuliaji wa timu ya Kipanga, Yunus Benard (katikaka) akichuana na mabeki wa timu ya timu Chuoni jana katika Uwanja wa Amaan. 

  Kipanga ilianza kipindi cha pili kwa kupeleka mashambulizi langoni mwa Chuoni ambao  walioneka wazi kuwa bado hawajakaa sawa na kuandka bao la kwanza katika  dakika ya 51, baada ya mchezaji Mohammed Abasi,  kujifunga katika harakati za kutaka kuokoa.
  Kuingia kwa bao hilo, maustadhi waa Chuoni ambao msimu uliopita walikamata nafasi ya pili walicheza bila ya malengo na kujikuta wakipachikwa bao la pii kunako dakika ya 60, baada ya mchezji, Imran Abdul, kufumua shuti lilokwenda moja kwa moja wavuni.
  Ligi hiyo  itaendelea tena leo katika viwanja viwili ambapo uwanja wa Amaan, maafande wa Polisi watacheza na Malindi  wakati kwenye dimba la Gombani Pemba, Hard Rock itapimana na Mtende Ranger.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIPANGA YAITUNGUA CHUONI 2-0 AMAAN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top