• HABARI MPYA

  Sunday, September 28, 2014

  MAZEMBE YATOLEWA KWA MABAO YA UGENINI, FAINALI NI AS VITA NA SETIF LIGI YA MABINGWA

  NDOTO za TP Mazembe kwenda Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, hii leo zimeota mbawa baada ya kutolewa na ES Setif ya Algeria kwa mabao ya ugenini kufuatia sare ya jumla ya 4-4.
  Setif walishinda 2-1 Algeria wiki iliyopita na leo, Mazembe wameshinda 3-2 mjini Lubumbashi- maaba yake timu ya Algeria inakwenda kuumana na AS Vita ra DRC pia mwezi ujao.
  Mabao ya Mazembe leo yamefungwa na Mghana, Daniel Adjei Nii dakika ya 21, Salif Coulibaly wa Mali dakika ya 38 na Jonathan Bolingi dakika ya 53, wakati ya Setif yamefungwa na Abdelmalek Ziaya dakika ya tisa Sofiane Younes dakika ya 75.
  Poleni vijana, haikuwa bahati yenu; Watanzania wanaochezea TP Mazembe, Mbwana Samatta kushoto na Thomas Ulimwengu kulia
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAZEMBE YATOLEWA KWA MABAO YA UGENINI, FAINALI NI AS VITA NA SETIF LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top