• HABARI MPYA

  Thursday, September 25, 2014

  MHAITI WA AZAM FC NJE WIKI MBILI, KANYAGIO LAKE LAPATA PANCHA

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI wa Azam FC, Leonel Saint-Preux atakuwa nje kwa wiki mbili kwa sababu ya maumivu ya kwenye unyayo wa mguu wa kushoto.
  Daktari wa Azam FC, Mbarouk Mlinga amesema kwamba mchezaji huyo wa kimataifa wa Haiti atahitaji uangalizi wa karibu katika kipindi chote cha mapumziko yake ili apone vizuri.
  “Ni tatizo dogo, ambalo linahitaji uangalizi wa karibu na mapumziko wakati matibabu yakiendelea,”amesema Dk Mbarouk.
  Leonel Saint- Preux atakuwa nje wiki mbili

  Leonel hakuichezea Azam FC katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Jumamosi Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam mabingwa hao watetezi wakianza na ushindi wa 3-1 dhidi ya Polisi Morogoro.
  Lakini alikuwepo kikosini wakati Azam FC inalala 3-0 mbele ya Yanga SC Septemba 14 katika mchezo wa Ngao ya Jamii, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Leonel atakosa mechi zisizopungua tatu zijazo wakati akiuguza maumivu yake kuanzia mchezo wa Jumamosi dhidi ya Ruvu Shooting Chamazi, Azam na Prisons mjini Mbeya Oktoba 4 na Azam na Mbeya City Oktoba 11, kama hautaahirishwa.
  Michezo ya Oktoba 11 na 12 inaweza kuahirishwa yote kupisha mechi ya kimataifa kati ya Tanzania na Benin Oktoba 12, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na mabadiliko yanatarajiwa kutangazwa kesho. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MHAITI WA AZAM FC NJE WIKI MBILI, KANYAGIO LAKE LAPATA PANCHA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top