• HABARI MPYA

  Tuesday, September 30, 2014

  MAJERUHI WAONGEZEKA AZAM FC, MWANTIKA FRIDAY NAO NJE, TIMU YAONDOKA KESHO KUWAFUATA PRISONS WALIOITOA JASHO YANGA SC

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  ORODHA ya majeruhi imeongezeka kwa mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Azam FC kufuatia wachezaji wengine wawili kuumia.
  Hao ni beki David Mwantika aliyeumia kifundo cha mguu katika mechi ya ligi hiyo na Ruvu Shooting na Kevin Friday ambaye anasumbuliwa na maumivu ya misuli.
  Azam FC inaondoka kesho Dar es Salaam kwenda Mbeya kwa ajili ya mchezo wake wa kwanza wa ugenini Ligi Kuu dhidi ya wenyeji Prisons Jumamosi, Uwanja wa Sokoine.
  Hata hivyo, Meneja wa Azam FC, Jemedari Said Kazumari amesema kwamba Mwantika na Friday wanaingia kwenhye orodha ya majeruhi wa timu, lakini kwa bahari nzuri maumivu yao si ya muda mrefu.
  Kikosi cha Azam FC kitaondoka kesho kwenda Mbeya

  “Hawa vijana wote watakuwa nje kwa wiki moja tu. Tukirudi kutoka Mbeya, naamini watakuwa wako fiti tayari na kuungana na wenzao,”amesema.
  Tayari Azam FC inawakosa Nahodha wake, John Bocco ‘Adebayor’, Frank Domayo, Joseph Kimwaga na Leonel Saint Preux, ambao wote ni majeruhi pia.
  Azam FC imeanza vyema mbio za kutetea taji lake msimu huu, baada ya kushinda mechi mbili mfululizo za awali, kwanza 3-1 dhidi ya Polisi Morogoro na baadaye 2-0 dhidi ya Ruvu Shooting, mechi zote zikipigwa Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Prisons pia inarejea Mbeya ikitokea Dar es Salaam baada ya juzi kufungwa 2-1 Yanga SC Uwanja wa Taifa, ikicheza pungufu kwa zaidi ya dakika 50 baada ya beki wake, Jacob Mwakalobo kutolewa kwa kadi nyekundu kipindi cha kwanza. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAJERUHI WAONGEZEKA AZAM FC, MWANTIKA FRIDAY NAO NJE, TIMU YAONDOKA KESHO KUWAFUATA PRISONS WALIOITOA JASHO YANGA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top